Inatokea sasa hivi: Hafla ya ufunguzi wa chuo kikuu cha Ameed…

Maoni katika picha
Katika mazingira yaliyo jaa bashasha na furaha yanayo endelea saa hizi katika hafla ya ufunguuzi wa chuo kikuu cha Ameed ambacho kipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwa huhudhiria kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na waziri wa elimu ya juu na utafiti wa kielimu dokta Abdurazaq Issa, pamoja na wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala pamoja na jopo la viongozi wa kidini, kisiasa na kitamaduni, pamoja na wawakilishi wa Ataba tukufu za Iraq ndani ya ukumbi wa chuo hicho.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikafuatiwa na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na kiongozi mkuu wa kiseria Sayyid Ahmadi Swafi, na ujumbe wa waziri wa elimu ya juu na utafiti wa kielimu dokta Abdurazaq Issa pamoja na ujumbe wa mkuu wa vyuo binafsi.

Katika hafla hiyo itaonyeshwa filamu inayo elezea kuanzishwa kwa chuo hicho, pamoja na vipengele vya kisheria, aidha washiriki watapata nafasi ya kutembelea mazingira ya chuo na kuangalia vyumba vya madarasa na maabara.

Kumbuka kua chuo cha Ameed ni taasisi ya kielimu ambayo ipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabat Abbasiyya tukufu, ina vitivo (michepuo) mitatu (Udaktari, Udaktari wa meno na Uuguzi) na kimesajiliwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, kinatarajiwa kutoa ushindani mkubwa wa kielimu, na kinafuata selebasi na kanuni za kimataifa zitakazo kiwezesha kua miongoni mwa vyuo bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: