Mkuu wa sekta ya elimu ya juu katika vyuo vikuu binasfi kutoka katika wizara ya elimu ya juu na utafiti dokta Ali Arzuqi Lamiy ameeleza kuridhishwa kwake na Atabatu Abbasiyya kujikita katika kutoa elimu ya udaktari kupitia chuo kikuu cha Ameed, akasema kua anamatumaini makubwa na wasimamizi wake, na kwamba wana uwezo mkubwa wa kufanikisha jambo hili.
Aliyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye hafla ya ufunguzi wa chuo kikuu cha Ameed, kilicho chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Juma Tano (10 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (29 Novemba 2017m).
Alisema kua: “Nafsi yangu imeridhika na inafuraha kubwa kusimama katika hafla hii tukufu, naupongeza ulimwengu wa kiislamu kwa kuingia wiki ya umoja wa kiislamu, wiki ya kuzaliwa kwa Mtume wa rehma na ubinadamu Muhammad (s.a.w.w), na wiki ya kutawazwa kwa Imamu wa zama (a.f), na jambo la tatu linalo nifurahisha zaidi ni ufunguzi wa chuo kikuu cha Ameed cha udaktari”.
Akaongeza kusema kua: “Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi pamoja na waziri wa elimu ya juu na utafiti dokta Abdurazaaq Issa, wamefanya juhudi kubwa kukamilisha maandalizi ya ufunguzi wa chuo hiki kitakacho changia sehemu kubwa katika sekta ya afya na kuokoa maisha ya watu”.
Akabainisha kua: “Kuna vyuo binafsi vingi hapa Iraq vilivyo leta maombi ya kufungua michepuo ya udaktari na tulikua tunafanyia kazi maombi yao, lakini baada ya kupata maombi ya Atabatu Abbasiyya watalamu wote wa wizara wametoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha swala hili linakamilika”.
Akamaliza kwa kusema: “Mradi huu usinge kamilika kama sio wale walio jitolea damu zao kwa ajili ya Iraq na maeneo yake matakatifu, hakika wao ndio sababu ya kufanikisha kwa miradi yote hii, nina imini na wasimamizi wa mradi huu, hakika wana uwezo mkubwa wa kufanikisha jambo hili tukufu Insha-Allah.