Miongoni mwao ni watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), Atabatu Askariyya tukufu yatoa zawadi kwa watu walio shiriki kufanikisha ziara katika msimu wa wafat wa Imamu Askariyyu (a.s)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa watu walio shiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa maimamu wawili -Askariyaini- (a.s), katika kipindi cha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Hassan Askariyyu (a.s) ni watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), Atabatu Askariyya tukufu imetoa zawadi kwa watu walio changia kufanikisha ziara hiyo, walio wakilisha Ataba mbalimbali na vikundi vya Husseiniyya, baada ya kukamilika kwa utoaji wa huduma zao katika ziara hii tukufu.

Shughuli ya utoaji wa zawadi hizo ilifanyika katika ukumbi wa utawala wa Atabatu Askariyya tukufu na kuhudhuriwa na mwakilishi wa uongozi wa Ataba Shekh Abdul-ghafaar Al-maaliki Imamu wa jamaa katika ukumbi wa haram tukufu ya Askariyya na kiongozi wa kitengo cha dini, ambaye alielezea furaha kubwa waliyo nayo kutokana na nyuso hizi tukufu zinazo wapenda Ahlulbait namna zilivyo fanya kazi kubwa kwa ajili ya kuwatumikia maimamu watukufu –Askariyaini- (a.s), na kuwakumbusha baadhi ya mazingatio, na kuelezea nafasi ya mujahidina (wapiganaji), hususan mashahidi waliopambana kukomboa mji wa Samara na kuimarisha usalama kwa mazuwaru watukufu, akahitimisha maelezo yake kwa machozi ya furaha na kuwaombea dua wadumu katika utumishi huu mtukufu.

Sayyid Hashim Mussawiy muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla hiyo alisema kua: “Daima tunajitahidi kutoa huduma katika sehemu hii takatifu tangu ilipo funguliwa haram hii tukufu katika matukio yote muhimu yanayo husu maimamu walio zikwa hapa, kwa maelekezo ya moja kwa moja kutoka katika ofisi kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hatuja wahi kufanya ubahili wa kutochangia katika utoaji wa huduma”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: