Atabatu Abbasiyya tukufu yaweka hema la Scaut kwa ajili ya huduma ya kwanza…

Maoni katika picha
Miongoni mwa juhudi zake daima za kuboresha huduma mbalimbali kwa mazuwaru watukufu, hususan zinazo fungamana na mambo ya kitamaduni na kielimu na kujenga maisha bora, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya watoto na makuzi iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni imeandaa hema la Scaut kwa ajili ya kutoa mafunzo ya namna ya kutoa huduma ya kwanza, yanayo fanyika kila siku ya Alkhamisi ya kila wiki katika mlango ya Kibla wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hema hili linalenga kutoa mafunzo kwa mazuwaru ya namna ya kujiokoa na kumuokoa mtoto anaye wezo kukosa pumzi katikati ya msongamano wa watu, jambo ambalo linaweza kutokea wakati wa kufanya ziara au hata katika maisha ya kawaida, pamoja na kutoa msaada kwa mtu aliye jeruhiwa au kukatika kiungo mambo yanayo tokea katika familia zetu, marafiki zetu na katika maisha kwa ujumla.

Kuhusu swala hili mkufunzi bwana Ali Auda amesema kua: “Kila siku ya Alkhamisi ya kila wiki tunatoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa mazuwaru watukufu, ambapo huwafundisha mazingira mbalimbali yanayo weza kutokea katika familia zao, marafiki zao na namna ya kutoa msaada wa awali na sio kuogopa na kuwa na hofu, tunajikita katika kuwafundisha mambo yafuatayo (Kupambana na majanga ya moto, kumsaidia majeruhi, au aliye katika kiungo, kumsaidia mwenye tatizo la presha, na kutoa msaada katika milio ya risasi)”. Mafunzo hayo tunatoa kwa watu wa rika zote.

Akaongeza kusema kua “Tunawafundisha kwa nadharia na vitendo, mtu tuliye mpa mafunzo huwa anashirikishwa moja kwa moja katika tukio halisi au kupitia mtu atakaye jitolea ili aweze kufanyia kazi yale aliyo fundishwa”.

Hema hili linapata muitikio mkubwa kwa watu wanaokuja kufanya ziara, huku wengi wao wakikiri kutokewa na matatizo na hawakujua namna ya kutoa huduma ya kwanza, kupitia hema hili wamepata ujuzi wa kupambana na mazingira korofi na namna ya kutoa huduma ya kwanza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: