Chuo kikuu cha Basra chaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na chathamini juhudi zake za kukisaidia…

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Basra kupitia mkuu wa kitivo cha malezi na elimu ya msingi dokta Hussein Auda Hashim, wameonyesha kuthamini mchango wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kusaidia taasisi za elimu ya sekula, katika juhudi zake za kuendeleza elimu nchini, msaada wao umeonekana wazi walipo saidia ujenzi wa kuongeza madarasa kupitia kitengo cha maarifa ya Qur’an kilicho fanya kazi kubwa ya kuendeleza swala hilo.

Dokta Hussein akaongeza kusema kua msaada wao kwetu sio katika hili tu, bali wametusaidia kifikra na wanatupa machapisho kutoka katika Ataba tukufu, hususan yanayo tolewa na kitengo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha ambampa baadhi ya vitabu vyake tunavitumia katika selibasi ya masomo.

Yalisemwa haya kufuatia ziara iliyo fanywa na watu kutoka katika Atabatu Abbasiyya wakiongozwa na mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha Shekh Dhiyaau-Dini Aali Majidi Zubaidiy na shekh Yasini msaidizi wa kiongozi mkuu wa turathi za Basra kwa mkuu wa kitivo cha malezi na elimu ya msingi katika chuo kikuu cha Basra.

Kumbuka kua ziara hii ilifanywa pembezoni mwa nadwa iliyo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika chuo kikuu cha Basra (kitivo cha malezi na elimu ya msingi ndani ya ukumbi wa Mji wa elimu, Juma Tano 29 – 11 – 2017m) iliyo husu kuutambulisha mradi wa utunzi bora kuhusu Qur’an tukufu kwa mujibu wa mwenendo wa vizito viwili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: