Baada ya kukombolewa mji wa Sanjaar kutoka katika himaya ya magaidi walio uharibu mji huo na miji mingine ya Iraq, na kujaribu kuondoa alama za dini na turathi, ujumbe kutoka katika idara ya maelekezo na msaada wa kimkakati kutoka katika kitengo cha dini chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wametembelea wilaya ya Sanjaar na kufika katika maqaam ya bibi Zainabu bint Imamu Sajaad na bibi Zainabu mkubwa bint Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), maqam hizo zipo katika eneo walipo ingizwa mateka kwa Somuah, Padri wa kikristo aliye shangazwa na kichwa cha Imamu Hussein (a.s).
Ugeni huo uliongozwa na Shekh Haidari Aaridhiy, waliondoa udongo na kufanya usafi katika malalo ya bibi Zaibab mdogo iliyo shambuliwa na magaidi wa Daesh.
Kisha wakaswali jamaa baada ya kutoa adhana kwa kutumia kipaza sauti kwa mara ya kwanza tangu mji huo kunajisiwa na magaidi ya Daesh.
Kuhusu ziara hii Shekh Aridhiy amesema kua: “Kutokana na chuki na uadui walio nao Daesh, wanafanya kila wawezalo kufuta alama zote zinazo ashiria utukufu wa Ahlulbait (a.s), magaidi hao walilipua malalo haya, na baada ya kuingia wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na kukomboa mji huu, tumemjulusha kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, naye ameagiza tufanye usafi katika eneo hili takatifu, kwa kushirikiana na ndugu zetu wa msaada wa kimkakati katika Hashdi Sha’abi na kutumia winchi zao na baadhi ya vifaa vyao tumeweza kusafisha eneo hili”.
Akongeza kusema kua: “Tunasubiri maelekezo yake yakujenga malalo hii au agizo lolote atakalo toa tupo tayali kutekeleza, tunatoa wito kwa kila mtu kuja kuwasaidia watu wa Sanjaar, hakika wanahitaji zaidi kusaidiwa kwani baada ya kurudi kwao hawajakuta kitu hata kimoja wanacho weza kunufaika nacho, magaidi ya Daesh yameharibu kila kitu”.
Shekh amewaomba watu wenye mamlaka na waumini wote na kila anae wapenda Ahlulbait (a.s), kusaidia kujenga upya Husseiniyya za Sanjaar zilizo haribiwa vibara na magaidi hao walipo kua wakikalia mji huu.