Utaratibu wa jarida la Rasdi unao fatwa na kituo cha kiislamu ni ule wa kunukuu tukio kama lilivyo tokea bila kuongeza wala kupunguza pamoja na kuangalia namna vyombo vya habari vilivyo ripoti tukio hilo, na kisha kuangalia kilicho nyuma ya pazia, kazi hiyo inafanywa na waandishi mahiri walio bobea, kisha wanakuja na msimamo wa kati bila kuegemea upande wowote,
Jarida hili lina waandishi nguli (walio bobea) katika sekta ya habari, na wamejikita katika mada kuu nne, ambazo ni:
- 1- Mada zinazo husu ulimwengu wa kiislamu.
- 2- Mada zinazo husu mchanganyiko wa tamaduni.
- 3- Mada zinazo husu Ushia na Mashia.
- 4- Mambo yanayo husu mambo ya Iraq.
Fahamu kua jarida hili halisambazwi sana, nalo linalenga kutoa mtazamo sahihi kwa watu wenye mamlaka na vyombo vya maamuzi, unapo tokea utata katika jambo lenye athari kwa jamii.
Ukitaka kuangalia zaiti kuhusu uandaaji wa jarida hili ingia hapa: http://www.iicss.iq/?id=38