Idara ya uhusiano wa vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu yaanzisha ratiba ya mjadala wa kitamaduni katika mashule na vyuo…

Maoni katika picha
Kathiratun (nyingi) ni ratiba inayo endeshwa na mradi wa kijana mzalando wa Alkafeel na kusimamiwa na idara ya uhusiano wa vyuo katika Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa ratiba hiyo ni hili lililo fanyika hivi karibuni kwa jina la (mjadala wa kitamaduni), ambalo ni muendelezo wa yaliyo fanywa miaka ya nyuma, na sasa linafanyika katika sura mpya na kwa upana zaidi, linahusisha shule za msingi sekondari maahadi na vyuo ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala.

Kuhusu ratiba hii Ustadh Azhar Rikabi kiongozi wa idara ya uhusiano wa vyuo amezungumza nasi akasema: “Mjadala wa kitamaduni ni kusambaza mbao vitakazo andikwa hadithi za Mtume na za maimamu wa Ahlulbait (a.s) zinazo husu malezi, akhlaq, elimu zitakazo saidia kujenga wanafunzi kiutamaduni na kukomaza uzalendo wa taifa lao, kwa kutumia uandishi mzuri unao vutia, na kufuata ratiba ya muda na sehemu kama ilivyo pangwa na idara, kuna mambo yanayo husu wanaume na wanawake tena yanayo endana na rika zao kiakili na kimasomo”.

Akaongeza kusema kua: “Mradi huu ni sehemu ya mradi mkubwa ulio andaliwa kwa lengo la kuinua uwezo wa wanafunzi katika elimu ya dini jambo ambalo litakua na matokeo chanya katika elimu kwa ujumla”.

Utawala wa shule, vyuo na Maahadi mbalimbali wamesifu na kupongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya jambo hili, na kusema kua lina umuhimu mkubwa katika kuwajenga wanafunzi kielimu, na wamesema kuwa hii ni njia rahisi ya kutoa elimu, kwani unaweza kuandika hadithi au kauli fulani ukasahihisha uwelewa wa jambo fulani na kujenga maarifa kuhusu jambo fulani na kuwafanya waende mlengo sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: