Kamati ya misaada kutoka ofisi ya Marjaa dini mkuu yatoa misaada kwa waathirika wa tetemeko katika mji wa Darbandakhaan na yawasaidia wakimbizi wa Huweijah vikapu 2300 vya chakula…

Maoni katika picha
Kamati ya misaada chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu haijaishia kusaidia wakimbizi na wapiganaji tu, bali imewasaidia waathirika wa tetemeko lililo tokea hivi karibuni katika wilaya ya Darbandakhaan na vijiji vinavyo zunguka wilaya hiyo katika mkoa wa Suleimaniyya, wamewapa misaada ya kibinadamu na vikapu 1700 vya chakula, mablanket elfu kumi pamoja na kuwafikishia salamu za pole kutoka kwa Marjaa dini mkuu na kuwaombea dua wao pamoja na wananchi wote wa Iraq wapate utulivu na amani.

Wamefikisha misaada hadi katika vijiji vya mbali kabisa milimani pamoja na ubovu wa barabara, sehemu zingine barabara ilikua imedondokewa na mawe makubwa lakini haikua sababu ya kuzuia msafara kwenda kutoa misaada ya kibinadamu.

Wanufaika wa misaada waliipokea kwa shangwe na furaha kubwa, wakashukuru sana kupata msaada huu kutoka kwa Marjaa dini mkuu, ambao unaonyesha kiasi kikubwa cha ubinadamu wake na nafasi yake kama baba wa raia wote wa Iraq, wakamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumuhifadhi na kumpa umri mrefu.

Katika tukio lingine kamati hiyo iligawa misaada ya vikapu 2300 vya chakula kwa wakimbizi wa Huweijah waliopo katika hema tatu za wakimbizi, baada ya kumaliza kugawa msaada huo, wakimbizi hao waliomba wafikishiwe salamu dua na shukrani zao kwa Marjaa dini mkuu, kutokana na ofisi ya Marjaa huyo kuwajali na kuwapa misaada ya mara kwa mara tangu wapatwe na tatizo la ukimbizi hadi sasa.

Kumbuka kua msafara huu ni sehemu ya mradi mkubwa unaotekelezwa na osiri ya Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh.w) wa kusaidia wakimbizi katika miji yote iliyo athiriwa na vita dhidi ya magaidi wa Daesh, pamoja na wakimbizi walio hifadhiwa katika mahema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: