Kwa kusaidiana na watalamu kutoka Ulaya: Alkafeel yaendesha mafunzo ya huduma ya kwanza vitani na namna ya kuhami watu mihimu…

Maoni katika picha
Watalamu wa Alkafeel wanaendesha mafunzo ya utoaji wa huduma ya kwanza na kulinda watu muhimu, katika mafunzo haya wameshiriki watu (15) kutoka katika kitebgo cha kulinda nidhamu na kitengo cha eneo la katikati ya haram mbilili tukufu, wamechaguliwa kutoka miongoni mwa wahitimu wa mafunzo yaliyo pita, katika mafunzo haya watasomeshwa mambo muhimu, pia wameshirikishwa watalamu kutoka Ulaya walio fundisha mbinu za kimataifa zinazo tumika Marekani kusini pamoja na mbinu za Iraq, na yalidumu siku tisa, kila siku saa (7 hadi 8).

Mtandao wa Alkafeel ulipata fursa ya kuongea na mmoja wa wakufunzi kutoka Ulaya bwana Tomasi Bill, ambaye alielezea kuhusu mafunzo haya kua: “Mafunzo haya yamefanyika katika baadhi za nchi zisizo kua na utulivu tena kila nchi yamefanywa kwa kufuata sheria na kanuni zao, nayo ni mafunzo maalumu kwa nchi zisizo kua na amani, kwa ajili ya kuwafundisha namna ya kulinda viongozi wao na raia wa kawaida, nayo ni mafunzo mazuri sana”.

Akaongeza kusema kua: “Namna mafunzo haya yanavyo fanywa ndio hivihivi pia hufanywa katika nchi za Ulaya, nivizuri nikabainisha kua, wanafunzi walikua na nidhamu nzuri sana, jambo hilo limetufanya tuweze kupunguza muda wa mafunzo hadi kubaki siku tisa, pia kutokana na uwezo wao mkubwa wa kuelewa haraka wanacho fundishwa”.

Kuhusu vipengele vya mafunzo haya bwana Tomasi amebainisha kua: “Mafunzo yamegawika sehemu tatu, sehemu ya kwanza ni mafunzo ya nadharia, sehemu ya pili ni mafunzo ya vitendo vya kuigiza yanayo husu namna ya kumuhami kiongozi na kumuingiza ndani ya gari, sehemu ya tatu ni mafunzo ya vitendo vinavyo fanana na mazingira halisi, baada ya mwanafunzi kufanya vizuri katika sehemu zote tatu ndipo anarudia tena kufanya sehemu zote kwa mara maja kama wanavyo fanya hivi sasa”.

Akaongeza kua: “Kuna sehemu ya nne pia ambayo inahusu namna ya kutoa huduma ya kwanza katika mazingira hatari ya vurugu au ya vita, au kumsaidia daktari katika mazingira tata, nayo ni sehemu muhimu sana katika mafunzo haya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: