Jarida la Ameed linaendelea kupasua anga, kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hivi karibuni kimetoa (awamu ya sita majarida ishirini na moja), likiwa limeshehena tafiti kumi na moja, miongoni mwa tafiti hizo ni; maendeleo ya kihistoria kuhusu mimbari Husseiniyya, nafasi ya mimbari katika kujenga uwelewa wa kidini na kijamii pamoja na misingi ya utambuzi kwa khatibu wa mimbari ya Hussein, tafiti zote zimeandikwa kiutalamu na zimekamilisha kanuni zote za kiuandishi.
Nakala hizi pia zimeandika mlango kamili unaosema (Mimbari ya Hussein ni mlango wa kukufikisha kwa Mtume (s.a.w.w)), kutokana na mambo yanayo patukana katika mimbari ya Hussein kua na nafasi kubwa ya kusambaza tamaduni za Ahlulbait (a.s), pamoja na changamoto inayo kumbana nazo za kifikra na kihabari, jambo ambalo limefanya kua lazima kwa khatibu wa mimbari ya Hussein awe na kila aina ya ukamilifu na ustahamivu.
Idadi ya tafiti iliyo tajwa –kumi katika hizo zimeandikwa kwa lugha ya kiarabu na moja imeandikwa kwa lugha ya kiengereza- uandishi wa tafiti hizo umefuata kanuni za lugha, jamii, dini, historia na saikolojia.
Kumbuka kua jarida la Ameed linatolewa na kituo cha masomo na utafiti cha Al-Ameed katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na linakibali cha wizara ya elimu ya juu na utafiti na limepasishwa kua chanzo cha upanuaji wa elimu, na limepewa namba ya kitaifa ifuatayo (ISSN: 2227-0346).