Kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya masomo: Atabatu Abbasiyya tukufu yaandaa mazingira ya shule katika mkoa wa Karbala…

Maoni katika picha
Mkoa wa Karbala sawa na mikoa mingine, una changamoto ya uchache wa majengo ya shule, pia zinahaja kubwa ya kufanyiwa matengenezo na ujenzi, miongoni mwa shule hizo ni shule ya Bayanu ambayo ipo chini ya uongozi wa malezi wa mkoa wa Karbala katika kitongoji cha Farihah, baada ya malalamiko ya wakazi wa eneo hilo kufika kwa viongozi wakuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, iliundwa kamati papo hopo ya watalam walio chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi, kwa ajili ya kwenda kufanya tathmini ya uharibifu uliopo katika shule hiyo na kuhakikisha wanaikarabati na kuandaa mazingira bora ya masoma.

Msimamizi mkuu wa matengenezo ya shule na naibu rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Samiri Abbasi Ali amesema kua: “Baada ya kufanya tathmini ya uharibifu katika shule hiyo na kuandika vifaa vinavyo hitajika kwa ajili ya matengenezo yake na kuukabidhi uongozi mkuu wa Ataba, uongozi huo ulibeba jukumu la kufanya matengenezo yote, ambayo ilikua ni kukarabati majengo ya shule, kupaka rangi kuta za majengo hayo, kukarabati njia za umeme na maji pamoja na vyoo, kurudia kuweka zege la paa na kuweka sakafu madarasani kwa kutumia aina bora za marumaru nyeupe, kurekebisha milango ya mbao na mingine kuibadilisha kabisa.

Wakazi wa kitongoji hicho na wadau wa elimu baada ya kuiona shule yao ikiwa katika muonekano mpya, wametoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya kutokana na kazi kubwa waliyo fanya ya kuwarekebishia shule hiyo tena kwa haraka na katika ubora mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: