Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa walimwengu: Korido zinazo ingia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimetandikwa mazulia mapya…

Maoni katika picha
Kufuatia kuingia kipindi cha furaha kwa waislamu kwa kuzaliwa kwa mbora wa walimwengu na Mitume Abu Qassim Muhammad (s.a.w.w), ulimwengu umejaa furaha kwa kuzaliwa kwake na mwezi unaangaza kutokana na nuru ya uso wake, kutokana na kuijiwa na uislamu ambao ni uongofu na rehma kwa walimwengu wote.

Kutokana na kumbukumbu hii tukufu kitengo cha uangalizi wa haram kwa kushirikiana na kitengo cha masayyid ambao ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wametandika mazuria ya fahari katika korido za milango inayo ilekea katika haram tukufu ya Abbasi hadi katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).

Zulia zilizo tandikwa zina upana sawa na zulia mbili zilizo pandanishwa, na zimetandikwa eneo lote ya korido, kwani zimetengenezwa kwa vipimo maalumu, mazulia hayo yanatofautiana urefu kutokana na eneo linapo tandikwa kati ya (4.5x3 mt), yamepanbwa nakshi nzuri zinazo endana na utukufu wa eneo hili, mazulia haya yana rangi nzuri inayong’aa tofauti na yale yaliyo tandikwa katika ukumbi wa haram tukufu.

Kumbuka kua milango ambayo korido zake zimetandikwa mazulia haya ni, mlango ya Kibla, mlango wa Imamu Hussein, mlango wa Furat (Alqamiy) na mlango wa Swahibu Zamaan, milango mingine imekua vigumu kutandika mazulia haya kutokana na kazi za marekebisho inayo endelea katika milango hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: