Mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya aelezea harakati muhimu na miradi ya Qur’an waliyo fanya…

Maoni katika picha
Mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Jawaad Nasrawi ameelezae harakati na miradi ya Qur’an waliyo fanya.

Aliyasema hayo katika ujumbe alio toa kwenye hafla ya kumaliza hatua ya kwanza ya mradi wa Qur’an kwa wanafunzi wa dini ulio endeshwa na Maahada hiyo, alisema kua: Kazi za Maahadi ya Qur’an tukufu zimegawanyika sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza: Kielimu, jukumu hilo linatekelezwa na kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, na wametekeleza miradi kadhaa, miongoni mwa miradi hiyo ni:

  • 1- Kuchapisha msahafu mtukufu, ambao kwa mara ya kwanza jambo hilo limefanika hapa Iraq.
  • 2- Mradi wa msahafu unao tamka tena kwa kufuata riwaya na visomo vya Ahlulbait (a.s), ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni nao unafanywa kwa mara ya kwanza pia hapa Iraq.
  • 3- Uchapishaji wa vitabu vya kusomeshea ambavyo baadhi ya vitabu hivyo vimepasishwa na kuingizwa katika mitaala ya shule za kiislamu na vyuo vikuu.
  • 4- Kuchapisha tafsiri ya Qur’an tukufu inayo jikita katika riwaya na maelezo ya watu wa nyumba tukufu ya Mtume (s.a.w.w).

Sehemu ya pili: Usomaji, sehemu hii inatekelezwa na kituo cha miradi ya Qur’an, na wamesha tekeleza miradi mingi, miongoni mwa miradi hiyo ni:

  • 1- Mradi wa semina za kipindi cha majira ya joto (kiangazi) kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari (upili), wamehitimu jumla ya wanafunzi elfu 16 katika semina zilizo pita, kutoka katika mikoa mitano.
  • 2- Mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, nao unalenga kugundua vipaji vya usomaji na kuviendeleza.
  • 3- Tumefanya zaidi ya semina 40 zinazo husu usomaji wa Qur’an na wamehitimu zaidi ya wanafunzi 350.
  • 4- Mradi wa mashindano ya usomaji wa Qur’an kwa vikundi, ilishiriki zaidi ya mikoa 11, ambayo hufanywa katika mwezi wa Ramadhani kila mwaka yakihusisha kuhifadhi, usomaji na tafsiri.
  • 5- Mradi wa kuhifadhi Qur’an tukufu, ambapo tumepata mahafidh 500 kuanzia juzuu moja na kuendelea.
  • 6- Mradi wa vituo vya Qur’an, ambao hufanywa katika kipindi za ziara ya Arubaini, katika ziara iliyo pita kulikua na zaidi ya vituo 130 vya usomaji wa Qur’an, kila kituo kilikua na maustadhi wanao fundisha usomaji wa Qur’an sura fupi fupi na surat Fat-ha pamoja na hukumu za Qur’an, walishiriki jumla ya maustadhi 450, wanufaika wa mradi huu ni zaidi ya watu (mazuwaru) laki tatu na elfu hamsini (350,000).
  • 7- Kuendesha semina za Qur’an kwa walimu wa Qur’an wa vyuoni.

Akaongeza kusema kua: “Na mradi huu ni miongoni mwa miradi ya Qur’an kwa wanafunzi wa dini hii ni hatua ya kwanza ambayo imehusisha utoaji wa mihadhara na nadwa kuhusu Qur’an, kutakua na hatua zingine zitakazo husisha usomaji wa Qur’an tukufu na kuhifadhi kwa kufuata maudhui”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: