Kufuatia kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume mtukufu, kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed kinafanya kongamano katika chuo kikuu cha Karbala…

Maoni katika picha
Kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na kitivo cha malezi na sayansi ya mwanadamu katika chuo kikuu cha Karbala wamefanya kongamano la kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume mtukufu asubuhi ya Juma Nne (16 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (5 Novrmba 2017m) chini ya kauli mbiu isemayo (Kwa utukufu wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) tunapata amani na tunaungana).

Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa kitivo (mchepuo) wa malezi na sayansi ya binadamu, lilihudhuriwa na mkuu wa kitivo hicho, pamoja na wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu hali kadhalika walimu na wanafunzi wa chuo pia walihudhuria kwa wingi. Hafla ya kongamano lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe wa mkuu wa chuo (kitivo) cha malezi na sayansi ya binadamu dokta Adnaan Mard Jibri ambaye alisema kua: “Hakika Mtume wetu mtukufu (s.a.w.w) alikuja kulingania tabia njema, lazima tupambike na tabia njema na kushikamana na mwenendo wake mtukufu na tufuate mwenendo wa watu wa nyumbani kwake (a.s), hafla hii tunayo fanya ya kukumbuka kuzaliwa kwake ni dalili ya wazi kua tunafuata sunna zake na kuzingatia mwenendo wake na tunatekeleza sheria zake”.

Mwisho dokta Adnaan alitoa shukrani zake kwa niaba ya chuo cha Karbala, akawashukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuwajali na kuja kufanya kongamano hili katika chuo hiki, tunatarajia jambo hili liendelee katika minasaba (matukio) mengine yajayo. Kisha ukafuata ujumbe wa kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed ulio wasilishwa na rais wa kitengo cha lugha ya kiarabu katika chuo kikuu cha Karbala dokta Ali Kadhim Maslawi ambaye alisema kua: “Leo tunasherehekea kuzaliwa kwa mbora wa viumbe, kipenzi cha Mola wa walimwengu Abu Qassim Muhammad (s.a.w.w), mtoto mtukufu, ambaye kuzaliwa kwake kulifungua ukurasa wa historia mpya, kukaondosha giza la jahiliyya na kuleta nuru ya uislamu, alikua msingi wa mabadiliko ya kweli katika nchi za uarabuni na akatengeneza jamii bora”.

Akaongeza kusema kua: “Katika mnasaba huu tunawakumbusha watoto wetu wanafunzi wajifundishe kutoka katika historia ya Mtume mtukufu namna ya kupambika na tabia nzuri, ukizingatia sasa hivi tunaishi katika zama zinazo jitahidi kupotosha umma wa kiislamu kifikra na kiitikadi”.

Vilevile ulitolewa muhadhara wa kielimu na dokta Abudi Judi Al-Hilliy aliye zungumzia historia ya Mtume (s.a.w.w) katika upande wa ubinadamu wake.

Hali kadhalika hafla ilipambwa na kaswida za kimashairi za kumsifu Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), na mwisho kabisa vilitolewa vyeti kwa baadhi ya washiriki na wasimamizi wa kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: