Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume mtukufu: Kumalizika kwa hatua ya kwanza ya mradi wa Qur’an tukufu kwa wanafunzi wa masomo ya dini…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa viumbe Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swaadiq (a.s), siku ya jana Juma Tatu Rabiul-Awwal 1439h, sawa na 4 Novemba 2017m, mradi wa Qur’an kwa wanafunzi wa dini ulio endeshwa chini ya usimamizi wa Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya tawi la Najafu ulihitimishwa.

Hafla ya kufunga mradi huo ilifanyika katika Husseiniyya ya Imamu Hassan Al-Mujtaba (a.s) katika mkoa wa Najafu na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na katibu wake mkuu, Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na wawakilishi kutoka katika ofisi za Maraajii dini watukufu, pamoja na idadi kubwa ya walimu na wanafunzi wa hauza na wanafunzi walio shiriki katika mradi huu.

Baada ya kusoma Qur’an tukufu pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, likafuatia tamko la ukaribisho kutoka katika Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, lililo tolewa na Shekh Jawaad Nasrawi, baada ya kutoa pongezi za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), alieleza mambo muhimu yaliyo fanywa na Maahadi tangu ilipo anzishwa hadi leo, pamoja na miradi ya baadae inayo tarajiwa kutekelezwa na Maahadi hiyo.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio wasilishwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi, ambaye alisifu utendaji wa Maahadi ya Qur’an tukufu, akionyesha namna wanavyo pambana kusambaza elimu ya Qur’an kupitia elimu ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), pia alihimiza kushikamana na kitabu cha Qur’an tukufu katika kila kitu ndani ya jamii zetu, hususan kwa wanafunzi wa dini na kwa msaada wa walimu watukufu wa hauza katika mji wa Najafu.

Halafu ukafuata ujumbe wa wanafunzi walio shiriki katika mradi huu, ulio wakilishwa kwa niaba yao na Shekh Daahil Khuzaaiy, alitoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na watu wote walio changia kufanikisha kwa mradi huu.

Mwisho wa hafla ziligawiwa zawadi kwa kila aliye changia kufanikisha kwa mradi huu, zilizo kabidhiwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi akishirikiana na viongozi wa hauza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: