Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, chuo cha Alkafeel chafanya kongamano la kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume mtukufu…

Maoni katika picha
Chuo cha Alkafeel katika mji wa Najafu chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwa kushirikiana na kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha mahusiano kupitia idara ya mahusiano ya vyuo katika Atabatu Abbasiyya wamefanya kongamano la kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume mtukufu lenye kauli mbiu isemayo (Tunajifaharisha kwa utukufu wa Muhammad na tunashinda kwa utukufu wa Muhammad), kongano hilo lilihudhuriwa na kiongozi mkuuwa wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi pamoja na wasomi wengi wa sekula na wa hauza.

Hafla ya kongamano hilo ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na dokta Ahmadi Kaabiy ambaye ni mjumbe wa kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed, miongoni mwa aliyosema ni: “Mtu hutahayari, kitu gani aseme? Na nini aandike? Katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume, hakika kila utakacho sema kuhusu Muhammad kitakua ni pungufu, na kila utakavyo msifu hauta maliza, hatutaki kurejea yaliyo semwa wala kuleta mapya, hakuna jipya kwa Muhammad zaidi ya kumpenda (s.a.w.w), wala hakuna jipya ambalo ni tukufu mno zaidi ya kumpenda, sisi hapa tunahuisha ahadi zetu na mapenzi yetu kwa Muhammad na tunajifunza upya kutoka kwake, nasi katika mwaka huu tunasherehekea kuzaliwa kwake tukiwa na visa mbali mbali, mwaka huu tumewashinda maadui wa Iraq, Mwenyezi Mungu amewatukuza waumini na kuwadhalilisha makafiri, hatukupata ushindi huo ispokua ni kwa kushikamana kwetu na mwenendo wa Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakasifu”.

Kisha ulifuata ujumbe wa chuo cha Alkafeel, ulio wasilishwa na mkuu wa chuo hicho dokta Nurusi Muhammad Dahaan ambaye alielezea utukufu wa Mtume (s.a.w.w), alisema kua: “Hakika Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni rehma iliyo letwa kwa walimwengu, Mwenyezi Mungu amemleta kwa watu wote pamoja na kutofautiana kwa mila, mataifa, rangi na jinsia zao, ni rehma kubwa iliyo letwa na Mwenyezi Mungu katika umbo la mwanadamu, ili macho yamuone na masikio yamsikie na nyoyo zimkubali na zipate utulivu kwake”.

Akaongeza kusema kua: “Enyi wahudhuriaji watukufu, katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa viumbe inayo endelea kufanywa na waislamu, tunapenda kusisitiza kua, sheria aliyo kuja nayo Mtume (s.a.w.w) inataka kujenga undugu na mapenzi baina yetu, tena sehemu zote na muda wote, nayo ni sheria inayo fundisha tabia njema, hakika Mtume (s.a.w.w) alikua na mambo makuu mawili, alisifika kwa matendo mazuri, na kadri muda unavyozidi kupita ndio ubora wa tabia zake unavyo zidi kuchanua”.

Pembezoni mwa kongamano hilo, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi alimpa zawadi dokta Swafaau Mussawiy kutokana na juhudi kubwa anayo onyesha katika uongozi wake kwenye chuo hicho (Alkafeel), na mmoja wa wanafunzi aitwaye (Ahmadi Hassan) alichora picha ya mmoja wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi, kisha baada ya hapo wakaanza kuimba mashairi ya kumpenda Mtume (s.a.w.w).

Kulikua na vikao vya kitafiti, ambapo zilihudhurishwa mada mbili, moja ilihudhurishwa na Shekh Swahibu Naswaar na nyingine ikahudhurishwa na Sayyid Muhammad Mussawiy, pia kulikua na maonyesho ya picha, na mwisho kabisa zikagawiwa zawadi kwa washiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: