Idara ya Qur’an chini ya kitengo cha mahusiano ya vyuo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendeleza ratiba yake ya mwaka jana, ya kufanya darasa mjadala (nadwa) kuhusu Qur’an chini ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, darasa mjadala hizo zinalenga wanafunzi wa vyuo na Maahadi hapa Iraq, kwa kuwasiliana na wakuu wa vyuo ili ratiba hii isigongane na masomo ya darasani.
Darasa mjadala hili, ni miongoni mwa utaratibu ulio wekwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unaolenga kujenga utamaduni wa kupambika na masomo ya Qur’an kwa wanafunzi wa vyuo, na kuchangia kujenga uwelewa wa wanafunzi wa vyuo kuhusu Qur’an tukufu na kuwafanya waweze kuakisi uwelewa huo katika maisha ya chuo, nyumbani au kwenye mazingira yanayo wazunguka.
Darasa mjadala hizi huendeshwa na mashekhe ambao huchaguliwa kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, na hupewa mada wanazo takiwa kuzisherehesha kwa kutumia aya za Qur’an na riwaya za maimamu wa Ahlulbait (a.s), baada ya kusherehesha mada husika, wanafunzi hupewa nafasi ya kuijadili na kuuliza maswali, ambapo hutakiwa kuuliza maswali ya moja kwa moja kwa mtoa mada au kwa kuandika kwenye karatasi, Shekhe aliye toa mada huwajibika kusherehesha na kujibu maswaali ya wanafunzi.