Ratiba iko kama ifuatavyo:
Siku ya kwanza: Kukusanyika katika kituo cha magari cha Maitham Tamaar na kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kwenda Madina na baada ya kuwasili huko watapewa vyumba vya kulala.
Siku ya pili: Kutembelea msikiti wa Mtukufu wa Mtume pamoja na makaburi ya maimamu (a.s) ya Baqii.
Siku ya tatu: kutembelea maeneo matukufu ya Madina (Mashahidi wa Uhudi – Masjid Qiblatain – Masjid Sab’ah – Masjid Kuba) pamoja na kutembelea bustani ya watumishi wa Imamu Hassan (a.s) na kutabaruku kwa kula chakula cha hapo.
Siku ya nne: Mapumziko na kutembea madukani.
Siku ya tano: Baada ya Adhuhuri msafara utaelekea Miqaat kwa ajili ya Ihraam katika Masjid Shajara/ na kuondoka hapo baada ya Magharib kuelekea Makka, baada ya kufika Makka watapewa vyumba vya kulala.
Siku ya sita: Kutekeleza ibada ya Umra, inajumuisha (Swala ya Tawafu – Sa’aiy baina ya Swafa na Marwa – Tawafu Nisaai – Swala ya Tawafu Nisaai).
Siku ya saba: Mapumziko na kutembea madukani.
Siku ya nane: Kutembelea maeneo matukufu ya Makka (Mlima wa Thuur - Arafaat – Muzdalifa - Minna – Mlima wa Nuur na mababuri ya Hajuun).
Siku ya tisa: Kufanya umra kwa niaba kwa watakao penda.
Siku ya kumi: Mapumziko na kutembea madukani.
Siku ya kumi na moja: Kurudi katika Nchi yetu kipenzi na tunatarajia kufika salama.
Ratiba ya safari inajumuisha mambo yafuatayo:
- -
- - Kukaa Madina siku nne (4).
- - Kukaa Makka siku sita (6).
- - Makazi ya Madina na Makka yatakua katika hoteli nzuri.
Gharama ya kushiriki katika safari hii ni:
- 1- Mtu mwenye umri wa (miaka 12 na zaidi) keshi ni ($875) na mkopo ($950).
- 2- Mtoto mwenye umri wa (miaka 2 hadi 11) keshi ni ($500) na mkopo ($600).
- 3- Mtoto anaenyonya mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja ($150).
- 4- Mtu atakaye hitaji chumba cha pili ($200).
Kutakua na mambo yafuatayo:
- 1- Msafara utafuatana na kiongozi wa idara na muelekezaji wa mambo ya dini.
- 2- Kila siku kutakua na milo mitatu katika kipindi chote cha safari.
- 3- Awasilishe paspoti ambayo bado inazaidi ya miezi sita ya kuendelea kutumika pamoja na picha tatu ndogo (paspoti size).
- 4- Mtu atakae penda kwenda umra kwa mkopo anatakiwa apate mdhamini mmoja miongoni mwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na atalipa deni kwa kukata pesa katika mshahara anaopewa na Alkafeel, na atatakiwa kutanguliza ($200) na atakatwa ($100) kila mwezi katika mshahara wake.
- 5- Gharama ya mtoto wa miaka miwili hadi kumi na moja (2 – 11) atatakiwa kutanguliza ($100) na atakatwa ($50) kila mwezi katika mshahara unaolipwa na Alkafeel.
- 6- Itaongezeka pesa ya kodi iliyo pangwa na serikali ya Saudi Arabia kwa wale waliofanya Umra katika kipindi cha mwaka 1438 hijiriyya. Kiasi cha Riali 2000 za Saudia.
Kwa maelezo zaidi: Wasiliana na kitengo cha kunufaika na mitambo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kilichopo katika eneo la mlango wa Bagdad kwenye jengo la Imamu Hassan Asakariyya (a.s), zamani likijulikana kama hoteli ya Dallah, au ofisi ya Saaqi iliyopo katika barabara ya Maitham Tamaar, au piga simu zifuatazo: (07801952463 au 07706091999).