Kitengo cha Mawakibu na Maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kimeshiriki pamoja na wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika wilaya ya Nu’maniyya kwenye mkoa wa Waasit katika sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binadamu na muongoaji wa umma Mtume Muhammad (s.a.w.w), na mjukuu wake Imamu Jafari Swaadiq (a.s), kushiriki kwao katika hafla ya maulidi, iliyo hudhuriwa na viongozi wa kidini, kisiasa, kijamii pamoja na ujumbe rasmi wa viongozi kutoka ngazi ya wilaya na mkoa.
Rais wa kitengo cha Mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan aliyeongoza msafara huo ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kupata mwaliko kutoka kwa watu wa Nu’maniyya tuliteuwa ujumbe utakao kwenda kushuriki katika sherehe ya maulidi ya Mtume pamoja na hafla ya ufunguzi wa Husseiniyya ya Saada Aali Khatiib, sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wengi wa dini akiwemo mwakilishi wa Marjaa dini wa mji wa Kadhimiyya Shekh Aali Yasini na Shekh Saadi Tamimi muwakilishi wa Marjaa katika mji wa Kuut pamoja na wawakilishi wa serikali ya eneo husika, na watu wengi wa mji huo”.
Akaongeza kusema kua: “Hafla ilipambwa na mihadhara mbalimbali iliyo elezea misingi ya ubinadamu aliyo kuja nayo Mtume (s.a.w.w), na umuhimu wa misingi hiyo kwa watu wa leo, pia kulikua na usomaji wa Kaswida na mashairi kuhushu kuzaliwa kwa Mtume na ushindi walio pata wanajeshi wa Iraq na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi wa Daesh”.