Marjaa dini mkuu ametahadharisha umma kupuuza misingi yake, amebainisha kua: “Hakika Qur’an tukufu ni kitabu cha uongofu na hekima yatupasa tunufaike nacho, jambo hatari zaidi ni pale inapo anza kupuuzwa baadhi ya misingi ya umma na asipatukane mtu wa kutahadharisha, na itakapo kua umma wenyewe ndio unao anza kupuuza na wala pasiwe na mkumbushaji, malipo yake yatakuaje? Bila shaka malipo ya duniani yatakua kama yaliyo tokea kwa umma wa Nabii Nuhu, Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo, na malipo ya akhera ni hatari zaidi na magumu zaidi wala hatuwezi kuyakwepa au kuyakimbia.
Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa (19 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (8 Desemba 2017m) iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Sayyid Ahmadi Swafi.