Jumuiya ya Scaut ya Alkafeel yafanya hafla ya kusherehekea maulidi ya Mtume mtukufu…

Maoni katika picha
Jumuiya ya Scaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Ijumaa (19 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (8 Desemba 2017m) wamefanya hafla ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari bun Muhammad Swaadiq (a.s).

Hafla hiyo iliyo fanywa katika ukumbi wa Imamu Ali Haadi (a.s) ilikua na mahudhurio makubwa ya wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wanachama wa Scaut.

Baada ya kusomwa Qur’an ya ufunguzi pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, na kuimbwa wimbo wa taifa pamoja na wimbo wa Ataba tukufu, ulifuata ujumbe wa Scaut ya Alkafeel ulio tolewa na dokta Maazin Kinani, baada ya salamu na kutoa pongezi kutokana na mnasaba huu alisema kua: “Huu ni mwaka wa nne mfululizo jumuiya ya Scaut ya Alkafeel inafanya maadhimisho ya maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swaadiq (a.s), tunapo sherehekea tukio hili hakika tunasherehekea sheria za Mwenyezi Mungu alizo kuja nazo, kuzaliwa kwake kulikua ni kukamilisha mlango wa Utume kwani yeye ndiye Mtume wa mwisho”.

Akaongeza kusema kua: “Tunasherehekea kuzaliwa kwa ubinadamu, kwani kabla ya utume wake jamii ilikua imejaa unyanyasaji mateso na umwagaji wa damu, leo alhamdu lillahi binadamu wameneemeka kutokana na tabia za Mtume (s.a.w.w) na kila zuli tulilo nalo linatokana na baraka pamoja na tabia nzuri alizo kua nazo Mtume mtukufu.

Akaendelea kusema kua: “Inatulajumu kujifunza kutokana na historia tukufu ya Mtume (s.a.w.w) katika nyanja ya tabia njema, ubinadamu, kijamii na kila nyanja ya maisha ya mwanadamu, naziomba familia tukufu wawahimize watoto kushikamana na tabia njema alizo fundisha Mtume na kuachana na fikra potofu zinazo pandikizwa katika jamii zetu”.

Hafla ilipambwa na Kaswida za kimashairi kuhusu mnasaba huu na kupongeza ushindi wa wanajeshi wetu na Hashdi Sha’abi, hali kadhalika palikua na onyesho la igizo lililo pewa jina la (Kuzaliwa kwa Nuru) lililo fanywa na vijana wa Scaut ya Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: