Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji watangaza kukamilisha jukumu walilo pewa, wamedhibiti na kufunga eneo la mwisho la mpakani baina ya Iraq na Sirya, asubuhi ya leo wapiganaji wa kikosi walielekea maeneo waliyo pangiwa na uongozi wa Hashdi Sha’abi kwa ajili ya kukomboa eneo la mwisho katika majangwa ya kisiwa kikubwa na juu ya mto Furat na kufunga mpaka baina ya Jamhuri ya Iraq na Jamhuri ya Sirya.
Katika opreshen hii wamekomboa zaidi ya kilometa (56) kwa urefu zikiwa zimegawika sehemu mbili, ndipo wakakutana na vikosi vingine vya ukombozi, miongoni mwa vikosi vya jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, hivyo aridhi yote ya Iraq tayali imesha kombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, na majeshi yetu yanadhibiti eneo lote la mpaka wa Iraq na Sirya kuanzia Waliid hadi Rabiah.
Naye kamanda wa vikosi maalum bwana Abdul-Amiri Rashidi Yara-Llah kiongozi wa opreshen ya kukomboa eneo hilo la kisiwa na juu ya mto Furat amesema kua: Hakika wapiganaji wa jeshi la serikali (Viongozi wa opreshen ya kisiwa – kikosi cha saba cha watembea kwa miguu – kikosi cha nane cha watembea kwa miguu na mitambo – kikosi cha tisa cha deraya) pamoja na vikosi vya Hashdi Sha’abi (1-20-25-26-31-33-40-41-44) wote kwa pamoja wamefanikiwa kukomboa eneo lote la kisiwa kilichopo baina ya Nainawa na Ambaar kwa kushirikiana na ndege za kivita za Iraq, wamefanikiwa kukomboa zaidi ya vijiji (90) na zaidi ya kilometa (16000) na wanadhibiti eneo lote la mpaka baina ya Iraq na Sirya kuanzia eneo la Rumana hadi Tal-Sufuk lenye urefu wa kilometa 183.
Kumbuka kua wajibu waliopewa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) ni kukomboa na kudhibiti eneo la mpakani linalo unganisha (Iraq – Sirya) na kufunga mpaka huo na kutangaza kua ni mstari mwekundu, na kutoruhusu kuvuka mpaka huo gaidi yeyote, vimeshiriki vikosi vyote vya wapiganaji katika vita hii.