Kuthibiti na kuhakiki: Kituo cha kimataifa cha masomo na utafiti Al-Ameed chatoa jarida la kumi na mbili kuhusu la hutuba za Ijumaa…

Maoni katika picha
Miongoni mwa machapisho ya kielimu yanayo tolewa na kituo cha kimataifa cha masomo na utafiti Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni jarida la hutuba za Ijumaa, leo limetoka jarida la kumi na mbili lenye zujuu la kwanza na la pili la mwaka 2016 miladiyya, jarida hili limekuja kakamilisha majarida ya awali na ni chachu ya majarida yatakayo endelea kutoka baada ya kuhakikiwa kielimu, ili kuyafanya majarida haya kua marejeo ya watafiti na wanafunzi wa elimu za juu.

Rais wa kitengo cha vitabu na majarida katika kituo cha Al-Ameed dokta Karim Hussein Naswihi Alkhaalidi, ameongea nasi kuhusu chapisho hili kua: “Baada ya kazi kubwa ya kuandika na kuhakiki iliyo fanywa na watalamu wetu usiku na mchana na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu leo tumefanikiwa kutoa mijaladi miwili ya hutuba za Ijumaa za mwaka 2016 miladiyya, mwaka ambao ulishuhudia utekelezaji mkubwa wa fatwa tukufu ya kujilinda na kupatikana ushindi wa haki dhidi ya batili”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika kukamilika kwa uhakiki na uandishi wa hutuba za Ijumaa za mwaka 2016m, ni mafanikio makubwa kwetu na yanatupa nguvu ya kuendelea na juhudi ya kuhakiki na kuandika hutuba za miaka mingine na kisha kuziweka mikononi mwa wasomaji na watafiti, kwani zinamada muhimu za Fiqhi, Usulu, Historia, Aqida, Siasa na Uchumi, zinafaa kusomwa na kufanyia utafiti kutokana na umuhimu wa mada zilizomo na hali halisi ya ulimwengu wa kiislamu, kwani mada zake zimezingatia mwenendo wa maimamu watakasifu (a.s) katika kutatua mambo ya kielimu na kufundisha uislamu halisi aliokuja nao babu yao Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kutoa mwanga katika mafundisho ya Qur’an tukufu kama walivyo tajwa na Mtume (s.a.w.w) kua wao ni kizito cha pili baada ya Qur’an tukufu”.

Alkhalidi akasema kua: “Hakika hutuba za Ijumaa zina nafasi kubwa inayo hitajiwa mno na wasomaji katika nchi za kiislamu, kwa ajili ya kufanyia utafiti fikra za maimamu watakasifu (a.s), kwani hutuba hizo zimejaa fikra tukufu na nukuu takatifu, pia kuna jambo muhimu sana linalo patikana katika hutuba hizo lalo ni kuenzi mwenendo wa maimamu (a.s), mradi huu una umuhimu mkubwa na nafasi ya pekee”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: