Sayyid Ashiqar aipongeza Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kufungua shule ya watoto yatima Sayyidat Ruqayyah…

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar ameipongeza Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kufungua shule ya watoto yatima Sayyidat Ruqayya ambayo ni msaada mkubwa kwa jamii na hasa watoto yatima.

Aliyasema hayo alipo ongoza ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika ufunguzi wa shule hiyo ulio fanyika leo Juma Pili (21 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (10 Desemba 2017m), iliyo hudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu Shekh Abdulmahdi Karbalai, ambaye alisema kua: “Ufunguzi wa shule ya awali Sayyidat Ruqayya unafanyika kutokana na Atabatu Husseiniyya kutilia umuhimu mkubwa swala la kutoa malezi ya kielimu kwa mayatima, ambao ni kundi kubwa katika jamii ya wairaq hususan mayatima wa mashahidi, tumeamua kulea kundi hili na kuwajengea mazingira mazuri ya kupata elimu sambamba na malezi bora baada ya kuwapoteza wazazi wao”.

Naye kiongozi mkuu wa shule za mayatima Sayyid Saadi-Dini Hashim Mahdiy alisema kua: “Atabatu Husseiniyya tukufu inamiliki shule nne za mayatima, shule ya msingi, sekondari (upili) na shule za awali, ya watoto wa kiume na ya watoto wa kike, shule hii inauwezo wa kupokea watoto wa kiume 250, wanapewa huduma za chakula, mavazi, usafiri, karatasi (vifaa vya kusomea) pamoja na huduma za afya”.

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, zinaipa umuhimu mkubwa jamii ya mayatima na zinawapa huduma mbalimbali, miongoni mwa huduma hizo ni kuwafungulia shule, vituo vya malezi pamoja na kuwapangia safari za mapumziko na kuwapa misada tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: