Miongoni mwa mfululizo wa miradi inayo husu Qur’an tukufu, ambayo inalenga kuimarisha utamaduni wa Qur’an kupitia harakati mbalimbali, kituo cha miradi ya Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinaendesha mradi wa mimbari za nuru, ambao unahusu kufanya mahafali na vikao vya kusoma Qur’an ndani na nje ya mkoa wa Karbala, katika maeneo ya Ataba tukufu au mazaru na katika Husseiniyya na misikiti, kwa kushiriki wasomaji wa Qur’an wa ndani na nje ya Iraq kwa mujibu wa ratiba.
Mradi huu umeanza kutekelezwa katika mkoa wa Misaan, imefanyika hafla ya Qur’an kwa kushirikiana na kikundi cha watumishi wa Qur’an na kizazi kitakasifu (a.s) na limeshiriki jopo la wasomi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kituo cha pili kilikua katika mazaru ya Shahidi Huru bun Yazidi Riyaahi, ndani ya mkoa wa Karbala, kwa kushirikiana na kikundi cha wasomi wa Qur’an wa eneo hilo pamoja na wanaotoka katika Ataba mbili tukufu Radhawiyya na Abbasiyya.
Mradi huu umepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa wasomaji na wadau wa Qur’an tukufu, wanaokuja kusikiliza usomaji wa Qur’an tukufu, hakika inasomwa katika sauti nzuri zaidi.