Kazi ya kutengeneza dirisha la mazaru ya Qassim mtoto wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s), inayo endelea katika kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi matukufu imepiga hatua kubwa kutokana na plani ya mafundi wanao fanya kazi hiyo.
Mafundi wanajuhudi kubwa katika undendaji wao, hatua ya kutengeneza umbo la mbao ni miongoni mwa hatua muhimu sana katika kazi hii, toka walopo pewa kazi ya kutengeneza dirisha wamefanya mambo mengi, kwanza kuchukua vipimo stahili, kukusanya dhahabu na fedha itakayo tumika katika dirisha hilo, na baada ya kupata vipimo kamili vya dirisha hilo ilifanyika kazi ya kuchagua aina ya mboa zitakazo tumika katika kutengeneza dirisha hilo.
Mbao iliyo chaguliwa kutumika ni mbao ya Swaaj Burmi, mbao hiyo ni imara zaidi, kwanza inauwezo wa kuvumilia mazingira tofauti ya majimaji na makavu, inauwezo mkubwa wa kubeba vitu vizito, hailiwi na wadudu wa aridhini na mengineyo, hivyo mbao hiyo ndiyo inayotumika kutengenezea dirisha hili.
Kazi ya kutengeneza umbo la dirisha imekamilika kwa kiwango kikubwa, na inafanyika ndani ya moja za kumbi za kiwanda hicho, uunganishaji wa vipande vya mbao umefanywa kitaalam zaidi tofauti na ulivyo kua ukifanywa katika madirisha mengine, limetengenezwa kama lilivyo tengenezwa dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s) ili kulifanya liweze kubeba madini ya dhahabu na fedha ambayo yanaendelea kuandaliwa sambamba na kazi hii.
Kumbuka kua uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliingia mkataba na mazaru ya Qassim bun Imamu Mussa bun Jafari (a.s) wa kutengeneza dirisha jipya la mazaru hayo, kazi hii imekua miongoni mwa miradi inayo tekelezwa na kiwanda hiki ya kutengeneza madirisha kama hayo, mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamesha pata uzowefu mkubwa wa kutengeneza madirisha ya aina hii, wamedhibitisha ufanisi wao pale walipo tengeneza dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s), lilikua dirisha la kwanza kusanifiwa na kutengenezwa kwa mikono ya wairaq, ili kuendeleza fani hii, Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua milango ya kutengeneza madirisha ya mazaru zingine, wamejipanga vizuri, ikiwa ni pamoja na kukusanya vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi ya kutengeneza madirisha ya kuweka katika makaburi matumufu na katika mazaru, kufuatia ufanisi na uzowefu mkubwa walio nao watalamu wake, wanaweza kutengeneza madirisha bora zaidi, mazuri na imara.