Kwa kushiriki Atabatu Abbasiyya tukufu, kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya chafungua maonyesho ya vitabu ya mwaka wa tatu…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumanne (23 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (12 Desemba 2017m), kitivo cha uhandisi kimefungua maonyesho ya vitabu ya mwaka wa tatu, ambapo mwaka huu yanafanyika chini ya kauli mbiu isemayo (Nimemaliza lakini nitaendelea kua muaminifu wa kitabu changu), ambayo Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki sambamba na Ataba zingine za (Alawiyya, Husseiniyya na Askariyya) pamoja na vyuo kadhaa na taasisi za usambazaji wa vitabu.

Maonyesho haya yanafanywa chini ya usimamizi wa rais wa chuo cha Mustanswiriyya dokta Swaadiq Hamash, tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limekua na ushiriki wa aina yake, kwa kuonyesha aina tofauti za vitabu vyenye faida kubwa kielimu vilivyo chapishwa na Ataba tukufu na kupangiliwa vizuri na ofisi ya maonyesho katika idara ya elimu na ubunifu chini ya kitengo cha habari na utamaduni miongoni mwa machapisho bora zaidi.

Rais wa chuo cha Mustanswiriyya dokta Swaadiq Hamash alipo maliza shughuli ya ufunguzi wa maonyesho hayo, alitembelea korido za maonyesho, akasifu sana ushiriki wa Ataba tukufu hususan Atabatu Abbasiyya, ambayo ilikua na mvuto wa pekee kwa wasomi wa kisekula na wanafunzi, Dokta Hamash amebainisha kua: “Hakika siku hizi ni miongoni mwa siku za furaha kwetu sote, kutokana na fatwa ya Marjaa wetu na ujasiri wa jeshi letu pamoja na Hashdi Sha’abi, sambamba na umoja wa raia na hekima za viongozi wetu, walio tuongoza hadi tukapata ushindi na kulifanya taifa hili kua la kwanza lililo weza kuwashinda magaidi wa Daesh walio kuja kufanya unyama na uharibifu katika taifa letu”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika tunacho shuhudia hivi sasa ni harakati za maendeleo mazuri ya elimu ya sekula katika taifa letu, jambo linalo ashiria kujenga mazingira mazuri kwa walimu na wanafunzi wetu, jambo litakalo saidia taifa letu kuo bora kielimu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: