Kitengo cha miradi ya kihandisi: Chakamilisha hatua kuu katika mradi wa upanuzi wa maqam ya Imamu Mahdi (a.f).

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya kumwaga zege kwenye paa katika mradi wa upanuzi wa maqam ya Imamu Mahdi (a.f), kazi inayo fanywa na shirika la ujenzi la Aridhi tukufu chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekamilisha umwagaji wa zege katika kupaua paa sehemu ya pili katika upande wa wanaume, lenye ukubwa wa mita za mraba (310) pamoja na ukumbi wa watumishi wenye ukubwa wa mita (150).

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya amebainisha kua: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu sasa hivi tumemaliza hatua kuu, ambayo ni hatua ya msingi, nguzo na umwagaji wa zege katika pande mbili za mto, kisha tumepandisha jengo na kukamilisha ujenzi wa paa la kwanza na sasa hivi tumekamilisha paa la pili na tumeanza kazi ya kukata madirisha sambamba na kazi zingine”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika kazi hizi zinatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na ufuatiliaji makini, hii inatokana na kufuatisha ratiba ya utekelezaji wa mradi, na tunajitahidi kukamilisha haraka kutokana na umuhimu wa sehemu hii hasa katika kipindi cha ziara za mamilioni ya watu”.

Fahamu kua maqamu ya Imamu Mahdi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya unapo ingia katika mji mtukufu wa Karbala kwa kupitia barabara inayo kwenda katika maqam ya Imamu Jafari Swaadiq (a.s), nayo ni mazaru (sehemu) mashuhuri, Atabtu Abbasiyya tukufu imechukua jukumu la kuikarabati na kuifanyia upanuzi kuanzia katika kubba lake hadi katika kumbi za haram na sehemu zingine za jengo hilo, kwa kua jengo hilo haliwezi kufanyiwa upanuzi katika pange zake tatu, imebidi upanuzi wake ufanye upande wa mto, ambao ni upande wa magharibi, kwa kutengeneza mfano wa daraja na kumwaga zege bila kuathiri njia ya mto, jumla ya eneo lililo ongezwa linafika mita za mraba (1200) na linafikika kwa kutumia njia na milango maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: