Ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Alkhamisi ya (25 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (14 Desemba 2017m), Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala pamoja na viongozi wa vituo vya afya kutoka katika mikoa mingine ya Iraq wameendesha warsha kuhusu namna ya kupambana na maradhi ya saratani.
Mkuu wa idara ya utambuzi wa mapema na kinga ya saratani katika wizara ya afya aliyekua mtoa mada katika warsha hiyo dokta Sanaa Abdurazaq Mansuur amesema kua: “Warsha hii inalenga kuweka mikakati ya kudhibiti saratani mapema na kutumia kinga, hasa saratani ya matiti ambayo inasambaa kwa kiasi kikubwa kwa wanawake, kiwango cha waathirika wa saratani ya matiti kinakaribia kufika nusu ya kesi tulizo pokea, tunavituo vya kuhama hama, vinavyo toa huduma ya kupima matiti kwa kutumia mionzi katika miji mbalimbali hapa Iraq, pamoja na kukusanya orodha ya waathirika wa saratani na kuwafafanulia njia za kujikinga na maradhi hayo”.
Akaongeza kusema kua: “Warsha imedum siku tatu, inalenga kuonyesha ukubwa wa tatizo kwa jamii na kuongeza uwezo wa wahudumu wa vituo vya afya, na kuangalia changamoto wanazo kutana nazo wahudumu wa vituo vya afya katika mikoa yote ya Iraq, na kutoa elimu kuhusu namna ya kuitambua mapema saratani ya matiti na namna ya kujikinga nayo, pamoja na kuangalia sababu kuu za kupata maradhi hayo, ambapo miongoni mwa sababu hizo ni za kimazingira na sababu zingine ni kutokana na baadhi ya vyakula au baadhi ya staili za maisha ya watu, pamoja na kubainisha njia za kujikinga na maradhi haya hatari”.
Katika warsha hii yamejadiliwa maoni mbalimbali kuhusu namna ya kupambana na maradhi haya bamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kupambana na maradhi yaha inayo weza kutekelezeka katika mazingira halisi.