Hivu punde, Marjaa dini mkuu: Hakuna utukufu kwa yeyote ispokua ni kwa wairaq wote ndio mlio fanikisha ushindi, ushindi umetokana na nyie ni wa kwenu! Nyie ndio washindi, hongereni sana…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu amebainisha kua hakuna mtu yeyete aliye leta ushindi ispokua wairaq wote ndio mlio leta ushindi, na ushindi ni wenu, hongereni sana, mmebarikiwa na kubarikiwa juhudi za kila aliye itikia wito na akatoka kupigana au akaunga mkono kwa namna yeyote ile, nyie ndio fahari yetu na utukufu wetu, na mtapongezwa na kila umma.

Hayo yalisemwa katika hkutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya (26 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (15 Desemba 2017m) iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Shekh Abdulmahdi Karbalai, ambaye alibainisha kua:

Enyi wairaq watukufu

Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya vita kali, mliyo jitolea kila kitu na mkapambana na mitihani mbalimbali, hatimaye mmewashinda magaidi walio ivamia Iraq, mmefelisha ndoto zao malengo yao na matarajio yao, mmewashinda kutokana na kujitolea kwenu nafsi zenu, na nafsi za wapenzi wenu pamoja na kila mnacho miliki, mlijitolea kwa ajili ya taifa lenu tukufu, hakika mmeweka historia ya pekee ya ushujaa na kujitolea, mmeandika historia mpya ya Iraq kwa utukufu wenu, ulimwengu umefadhaishwa kwa ujasiri wenu na subira yenu, na namna mlivyo pambana kwa uadilifu hadi mkapata ushindi huu mkubwa, ambao wengi walidhani kua usinge patikana, lakini nyie mmefanikisha kwa muda mfupi, mmelinda utukufu wa taifa lenu na kuthibitisha umoja wa taifa lenu hakika nyie ni watu watukufu mmno.

Enyi wapiganaji watukufu, enyi wapiganaji wa vikosi vyote na majeshi yote, hakika Marjaa dini mkuu aliye toa fatwa ya wajibu wa kujilinda, iliyo tengeneza mazingira na kujenga moyo wa kupigana, pamoja na kujitolea watoto bora ambao ni wanafunzi wa hauza na walimu wao kwenda kuungana na wapiganaji katika uwanja wa vita, na kuuawa mashahidi wengi katika vita hizo, haoni yeyote mwenye utukufu kama wenu wala anaye paswa kusifiwa kama nyie katika kufanikisha ushindi huu muhimu wa kihistoria, kama sio kuitikia kwenu fatwa ya Marjaa na kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa vita, pamoja na kusimama kwenu imara na kupigana kwa ushujaa na ujasiri mkubwa kwa zaidi ya miaka mitatu usinge patikana ushindi huu, ushindi umetokana na nyie na ushindi ni wenu, hongereni sana, mmebarikiwa na kila aliye shiriki kwa namna moja au nyingine pia kabarikiwa, nyie ni fahari yetu na utukufu wetu mtapongezwa na kila umma.

Utukufu ulioje kwa Iraq, hakika mlijitolea roho zenu kwa ajili ya kulinda taifa lenu na maeneo yake matukufu, hakika hatuwezi kuwalipa baadhi ya haki zenu, lakini Mwenyezi Mungu mtukufu atawapa malipo makubwa, hatuna la kufanya kwenu ispokua kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu akuzidishieni baraka na akulipeni malipo mema.

Enyi kaka zangu na dada zangu, hakika tunawakumbuka kwa unyenyekevu mkubwa mashahidi wetu watukufu, walio lowanisha udongo wa taifa hili kwa damu zao tukufu, walikua mfano mkubwa katika kupigana na kujitolea, tunasimama pamoja na familia zoa katika kuwakumbuka, baba zao, mama zao, wake zao, watoto wao, kaka zao na dada zao, hawa ni watu watukufu mmo kwetu kwani waliwaruhuru wapenzi wao na wakaonyesha subira ya hali ya juu kabisa. Na tunawakumbuka kwa unyenyekevu mkubwa ndugu zetu majeruhi, hususan walio pata ulemavu wa kudumu, hakika wao ni mashahidi walio hai, Mwenyezi Mungu amependa waendelee kubakaia pamoja nasi na kutupa ushuhuda kuhusu ushujaa wao katika uwanja wa vita na namna walivyo washinda maadui. Pia tunawakumbuka na kuwashukuru sana raia wote wa Iraq walio simama imara na kuwapa misaada mbalimbali wapiganaji watukufu katika uwanja wa vita, hakika walikua ni wasaidizi wema kwa wapiganaji, mlionyesha umoja na mshikamano katika kuwasaidia wapiganaji, pia tunawakumbuka na kumshukuru kila aliye saidia katika sekta ya kutoa elimu, tiba, habari, mashairi, kuandika kitabu, Makala, kipeperushi na vinginevyo. Tunatoa shukrani za dhati kwa kila mtu aliye simama pamoja na wairaq katika kipindi huki kigumu cha mtihani wa magaidi wa Daesh, na kutoa msaada wa aina yeyote, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awaondelee aina zote za shari na awaneemeshe kwa kuwapa amani na usalama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: