Marjaa dini Shekh Fayaadh atoa tamko kua ushindi umepatikana kwa mambo mawili: Fatwa ya Marjaa dini mkuu na mwitikio wa wairaq wa fatwa hiyo…

Maoni katika picha
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na rehma na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na Aali zake watakasifu…

Mwenyezi mungu anasema: (Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanaume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi. Basi walio hama, na wakauliwa, kwa yakini mimi nitawafutia makossa yao, na kwa yakini nitawaingiza katika mabustani yanayo pita mito kati yake. Hayo ndiyo malipo yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu kwake yapo malipo mema kabisa) Al-Imraan: 195.

Amani iwe juu yenu watu wenye subira mujahidina raia wa Iraq watukufu…

Tupo katika siku za kusherehekea tukio tukufu sana katika roho zetu na zenu, tukio tukufu linalo burudisha nafsi zetu, kwa nini tusifurahi wakati tunakumbuka kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), pia zimekua siku ambazo furaha imeongezeka mara dufu, kwani zimesadifu ushindi wa jeshi na wapiganaji wetu dhidi ya magaidi wa Daesh waliotaka kuzima mwanga wa jua kwa dhulma zao, na kusababisha mitihani na matatizo tele.

Tunawapongeza sana kwa kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume mtukufu, Tuna muomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kufuata mwongozo wake, na atupe uwelewa zaidi katika dini yetu, na kua waja wema wanao pambana na waovu kwa kauli na vitendo, na kuwa wamoja katika kutetea haki.

Enye ndugu: Hakika fitina ya magaidi wa Daesh pamoja na vibaraka wao, tusinge ishinda kama sio mambo mawili makuu:

Jambo la kwanza: Umakini wa Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu, na uwezo mkubwa wa kukadiria hatari ambayo ingesababishwa na magaidi, kutokana na uzowefu wa miaka mingi, pamoja na hekima kubwa iliyo ambatana na kuelewa mazingira ya umma kihistoria, na utashi wa kweli walio nao raia wa taifa hili, na kuzuia kuvunja imani zao, ndipo ukawa msimamo wa Marjaa dini mkuu ni kumtaka kila anaye weza kubeba siraha afanye hivyo na kupambana na hatari ya magaidi wa Daesh, ikawa sawa na kuifanyia kazi kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa, na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwasaidia (39). Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kua wanasema: Mola wetu mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za watawa na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu Mtukufu). Surat Hajji: 39 – 40.

Pia akawashajihisha wanafunzi wa hauza kushiriki katika uwanja wa vita, kwa ajili ya kuongeza ari zaidi ya wanajeshi na wapiganaji wote kwa ujumla, na kutoa mashahidi wengi waliopata utukufu wa elimu, jihadi na shahada.

Jambo la pili: Mwitikio mkubwa na wa haraka kutoka kwa raia wa fatwa ya jihadi ya kujilinda, katika hali nzuri kabisa watu wamejitolea na wamefikia malengo, kila mtu alionyesha utayali wa kujitolea mali zote na nafsi yake, hadi kupatikana ushindi, subira yenu na jihadi yenu zimezaa matunda, na kupatikana faraja baada ya dhiki. Hili sio jambo geni kwenu, mmekua watu wa kwanza kujitolea katika mambo matukufu, ushujaa mmerithi kwa babu zenu, ambao hawakukubali dhulma na uonevu, walipambana hadi wakaishinda batili na kuiondoa kabisa, bila shaka vita ya Ishirini sio ngeni kwenu. Tunatoa shukrani za dhati kwa kila mtu aliye saidia au kusimama pamoja na wairaq katika kipindi kizito cha matatizo, pia nakumbusha jukumu la viongozi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na mbele ya raia hawa wadhulumiwa, wanajukumu la kujenga maelewano baina yao na kuunda serikali yenye misingi imara ya kutenda haki, pamoja na kuchagua viongozi waaminifu na wachapa kazi, na kuondoa upendeleo wa vyama na vikundi, ili serikali iweze kuendesha mambo yake kwa haki na uadilifu, na kuitoa nchi katika mazingira haya mabaya, pia iangalie namna ya kupunguza mishahara na baadhi ya stahili za vigogo, kuhusu swala la kupambana na ufisadi ni zuri lakini kama misingi ya utawala haita badilishwa hali itaendelea vile vile.

Mwisho tunasema: Enyi wananchi watukufu: Hakika tunakutakieni mustakbali mzuri, na tunaomba muwe kitu kimoja, muwe na kauli moja, msimame safu moja, mnufaike na utulivu wenu, amani ienee katika nchi, mlinde misingi yenu na dini yenu pamoja na utaifa wenu, bila kusahau maeneo yenu matukufu, Mwenyezi Mungu ayape nguvu mazuri yenu na afelishe njama za adui zenu.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu na rehma zake na baraka zake…

Muhammad Is-haqa Fayaadh

Rabiul-Awwal 17/ 1439h.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: