Kwa kushiriki wanafunzi (2000): Ataba mbili tukufu zahitimisha semina za Qur’an kwa wanafunzi wa vyuo na Maahadi…

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Baabil kilikua mwenyeji wa semina za Qur’an kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iraq, zilizo endeshwa chini ya mradi wa Qur’an unao simamiwa na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na kushiriki wanafunzi (2000) kutoka katika vyuo na Maahadi tofauti.

Hafla ya kufunga semina hizo ilifanyika katika ukumbi wa Shahid Sayyid Muhammad Baaqir Swadri ndani ya chuo kikuu cha Baabil, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya walimu na wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi walio shiriki katika semina hizo.

Baada ya kusomwa Qur’an tukufu ya ufunguzi, ulifuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu ulio wasilishwa na mkuu wa Maahadi ya Qur’an katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Shekh Jawaad Nasrawi ambaye alisema kua: “Hakika Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) zilikua sawa na Ataba zingine, kua ni mahala pa kufanya ziara basi, hata hiyo ziara haikufanywa kwa uhuru, kwani mtu alikua anafanya ziara huku anaogopa kukamatwa na utawala uliopita (wa Sadam), baada ya kuanguka utawala huo, haki imerudi kwa raia, na uongozi wa Ataba umerudi kwa Marjaaa dini mkuu, sasa shughuli zote za Ataba ziko chini ya kiongozi anaye kubalika kisheria, kutokana na fursa kubwa waliyo nayo wasimamizi wa Ataba kwa sasa wameweza kuzifanya kuwa sehemu kuu za kutoa elimu ya dini”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika kila mita na kila ncha katika jengo la Ataba tukufu ni sawa na taa linalo angazia elimu na wana chuoni, kwa ajili ya kufikisha fikra za Ahlulbait (a.s) kwa walimwengu wote, tuna mshukuru Mwenyezi Mungu Ataba hizo kwa sasa zimefungua vitengo vingi kwa ajili ya kutoa elimu ya Ahlulbait (a.s), miongoni mwa vituo hivyo ni Darul-Qur’an iliyopo katika Atabatu Husseiniyya tukufu na Maahadi ya Qur-an iliyopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, lengo lao kuu ni kupandikiza elimu ya Qur’an na aqida katika nafsi za waumini, vitengo hivyo vinaendesha semina mbalimbali zinazo lenga makundi tofauti ya watu katika jamii, miongoni mwa semina hizo ni hii ambayo wamehitimu zaidi ya wanafunzi (300) wakike na wakiume kutoka katika chuo kikuu cha Baabil, na kushiriki zaidi ya wanafunzi (2000) kutoka katika vyuo vikuu vya Iraq”.

Uongozi wa chuo ulitoa shukrani nyingi kwa Ataba mbili tukufu kwa kuendesha semina hii tukufu ya Qur’an, yenye faida kubwa kwa wanafunzi wao.

Mwisho wa hafla wanafunzi walio shiriki katika semina wakapewa vyeti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: