Pamoja na aridhi kua tupu: Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji chasonga mbele katika safisha safisha mashariki ya Samara…

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinasonga mbele katika safisha safisha ya mji wa Matwibijah uliopo mashariki ya Samara, kwa kushirikiana na kikosi cha Maghawiri cha opreshen za mji wa Samara na kikosi cha (17) cha jeshi la muungano katika upande wa kusini, kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mji wa Samara na maeneo yanayo zunguka mji huo na kumaliza kabisa mabaki ya magaidi wa Daesh ambao hutumia maeneo hayo kufanya mashambulizi yao.

Kikosi kimefafanua kua, pamoja na aridhi kua tupu na ugumu wa kusonga mbele katika maeneo hayo, haikua sababu ya kuzuia kusonga mbele kwao, kikosi cha wahandisi kimefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wapiganaji wanasonga mbele na kudhibiti maeneo yote ya kimkakati, kikosi cha Abbasi kimekusudia kuwamaliza kabisa magaidi ambao bado wanatega mabomu na kujaribu kukwamisha juhudi zao, pamoja na hivyo majemedari wa Alkafeel wanaendelea kusonga mbele kama kawaida, viongozi wa wapiganaji wanasema kazi inaenda vizuri.

Kikosi kimebainisha kua, kimesafisha safisha zaidi ya kilometa (10) ndani ya mji wa Matwibijah mashariki ya Samara, pamoja na kijiji cha Ahmad Jaasim na kijiji cha Ramli hadi katika chuo cha Rami, na wamefanikiwa kuangamiza handaki la magaidi wa Daesh, ndege za kivita zinasaidia kusonga mbele kwa vikosi hivi, hadi wakati tunaandaa taarifa hii ilikua bado opreshen inaendelea.

Tunapenda kufahamisha kua kikosi cha Abbasi kwa kushirikiana na vikosi vingine wameanza opreshem hii leo asubuhi kwa lengo la kuimarisha usalama katika mji wa Samara na maeneo yanyo uzunguka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: