Marjaa dini mkuu awahutubia watu wa Iraq: Ulimwengu umeshangazwa kwa ujasiri, subira na msimamo wenu…

Maoni katika picha
Khutuba ya Ijumaa ya mwisho imebeba ujumbe mwingi, kila sehemu ya khutuba hiyo ni muhimu na inatengeneza historia ya umma.

Marjaa dini mkuu ametumia uwezo wake tangu kutolewa kwa fatwa ya jihadi ya kujilinda, amesimama pamoja na wapiganaji na kuwapa misaada na maelekezo, sambamba na kuwaruhusu wanafunzi na walimu wa hauza kuingia katika uwanja wa vita na wengi miongoni mwao kupata shahada, jambo lililo pelekea vikosi vyote vya jeshi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, na kuongezeka subira na ujasiri, na kutengeneza historia mpya ya Iraq iliyo jaa utukufu, kama alivyo sema Marjaa dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa iliyo pita (khutuba ya ushindi) akihutubia raia wa Iraq kua:-

“Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya vita kali, mliyo jitolea kila kitu na mkapambana na mitihani mbalimbali, hatimaye mmewashinda magaidi walio ivamia Iraq, mmefelisha ndoto zao malengo yao na matarajio yao, mmewashinda kutokana na kujitolea kwenu nafsi zenu, na nafsi za wapenzi wenu pamoja na kila mnacho miliki, mlijitolea kwa ajili ya taifa lenu tukufu, hakika mmeweka historia ya pekee ya ushujaa na kujitolea, mmeandika historia mpya ya Iraq kwa utukufu wenu, ulimwengu umeshangazwa kwa ujasiri wenu na subira yenu, na namna mlivyo pambana kwa uadilifu hadi mkapata ushindi huu mkubwa, ambao wengi walidhani kua usinge patikana, lakini nyie mmefanikisha kwa muda mfupi, mmelinda utukufu wa taifa lenu na kuthibitisha umoja wa taifa lenu hakika nyie ni watu watukufu mmno”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: