Atabatu Abbasiyya tukufu yaadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya Dhwaad…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni, imeadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya Dhwaad (lugha ya Kiarabu), kwa kufanya darasa mjadala (nadwa) ya kielimu, lililo fanyika chini ya ujumbe usemao (Kiarabu ni msingi wa utamaduni wetu na nguzo ya umoja wetu) katika ukumbi maalumu wa mikutano, na kuhudhuriwa na wasomi wa kisekula kutoka vyuo mbalimbali.

Ustadh Aadil naibu rais wa kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed ametuambia kuhusu nadwa hiyo kua: “Kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed kimeadhimisha siku ya Dhwaad kwa kuwakaribisha wabobezi wa lugha ya kiarabu ambao walizungumzia misamiati ya kiarabu na wakaelezea umuhimu wa kuhifadhi lugha ya kiarabu katika zama hizi za maendeleo yanayo tishia kuharibu lugha za watu wengi, mada kuu iliyo jadiliwa katika maadhimisho hayo ni kulinda lugha ya kiarabu”.

Naye dokta Twariq Abdu-Aun Janabi aliye kua miongoni mwa watoa mada katika nadwa hiyo alisema kua: “Katika mada yangu nimeandika mambo mengi, miongoni mwa mambo muhimu niliyo andika ni magonjwa ya lugha ya kiarabu na njia za kuyatibu, nimeandika pia namna ya kumuandaa mwalimu mwenye mafanikio, anaye endana na mazingira ya kukua kwa lugha na anaye weza kutumia zana za lugha, kwani humsaidia kuwa na lugha sahihi na faswaha, hakika kufanya nadwa za aina hii bila shaka kuna faida kubwa sana iwapo zitatumika vizuri”.

Dokta Karim Hassan Naaswih mmoja wa wajumbe wa kituo cha kimataifa Al-Ameed amesema kua: “Leo tumejadili umuhimu wa lugha ya kiarabu, pamoja na kuzingatia kua Qur’an tukufu imeteremshwa kwa lugha ya kiarabu, na kwamba lugha ya kiarabu inahistoria kubwa na imefaidisha umma nyingi, hali kadhalika tumebainisha mchango mkubwa uliotolewa na wazungumzaji wa lugha ya kiarabu katika sekta ya elimu mbalimbali ambazo zimenufaisha dunia nzima kwa ujumla”.

Akaongeza kusema kua: “Kwa hakika mimi nilionyesha uwiyano baina ya waarabu na juhudi zao na mambo yaliyopo katika lugha za sasa, ili kumuonyesha msikilizaji kua; kilicho fanywa na lugha ya kiarabu kina umuhimu mkubwa sana sawa na kinacho fanywa na lugha za kisasa, nikataja ushahidi kutoka katika kitabu cha Sibawaihi, ambacho ni kitabu kongwe zaidi, na kina mambo mengi yanayo tumika katika fani mbalimbali leo hii, jambo ambalo linaonyesha mchango wa lugha ya kiarabu katika maendelea na fikra za kisasa, na kwamba kiarabu kilizitangulia lugha zingine, sio kwamba ni asili ya lugha zingine tu bali turathi zake ni imara (kina misingi imara) ukilinganisha na lugha za kisasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: