Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi chakamilisha safisha safisha katika ngome ya mwisho ya magaidi wa Daesh kwenye mji wa Matwibijah na chaimarisha usalama katika maeneo yanayo zunguka mji wa Samara na Atabatu Askariyya tukufu…

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kimetangaza kukamilika kwa kazi ya safisha safisha katika mji wa Matwibijah na maeneo yanayo zunguka mji huo yanayo kadiriwa kua kilo mota (160).

Chini ya utekelezaji wa majukumu ya kivita, wapiganaji wa kikosi cha Abbasi wamefanikiwa kukamilisha msako na safisha safisha katika ngome ya mwisho ya magaidi wa Daesh kwenye maeneo hatari zaidi kutokana na jografia yake, wamefanikiwa kukomboa vijiji na kuharibu mahandaki pamoja na kudhibiti eneo lote la mji huo, kutokana na juhudi kubwa za blugedi ya wahandisi walio fanya kazi kubwa ya kuchonga barabara.

Kwa mujibu wa maelekezo ya makamanda, wameamua kubakiza katika mji wa Samara brugedi ya deraya na kikosi cha Alqami kwa ajili ya kulinda ushindi walio pata.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: