Miongoni mwa juhudi za kuboresha kilimo: Shirika la teknolojia ya kilimo Aljuud latengeneza mbolea ya (Dabu Taji Saail)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa juhudi zake katika kuboresha uzalishaji wa kilimo jambo linalo tafutwa sana na wakulima wa Iraq, na kufuatana na mazingira ya hali ya hewa pamoja na ardhi ya kilimo sehemu moja hadi nyingine hapa nchini, shirika la teknolojia ya kilimo Aljuud, lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limetengeneza mbolea ya (Dabu Taji Saail).

Mbolea hii inaingia katika orodha ya mbolea nyingi zilizo tengenezwa na shirika hili zinazo sifika kwa ubora mkubwa, zina kiwango cha juu cha kimea cha Fasfuur na zina Netrojen inayo endana na mazingira ya mashamba na kukubaliana na mimea na miti ya matunda.

Tofauti ya mbolea hii na aina zingine zilizopo sokoni, ni kwamba; mbolea hii inauwezo wa kustahamili mazingira tofauti na uwezo mkubwa wa kuto haribika au kuharibu mimea, pia haiharibu maji na inauwezo mkubwa wa kurutubisha mmea ulio dhoofika kutokana na kukosa rutuba katika ardhi, na inaongeza mavuno mara dufu.

Mbolea hii ni miongoni mwa mbolea zinazo fanyiwa uchunguzi mfululizo na watalamu wetu, kwa ajili ya kulinda usalama wa mimea na kuifanya iwe bora wakati wote kulingana na mazingira, imetengenezwa rasmi kwa ajili ya shamba banda (Green House) na mashamba ya wazi, ni nzuri kwa kurutubisha aina mbalimbali za mimea.

Fahamu kua Shirika la Aljuud linatengeneza vifaa mbalimbali vya kilimo pamoja na mbolea za aina tofauti na vitu vingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: