Katika khutuba ya ushindi: Marjaa dini mkuu ashukuru msaada wa wairaq kwa ndugu zao wapiganaji na walio wasaidia miongoni mwa ndugu na marafiki…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu hakuacha kutilia umuhimu –kupitia khutuba ya Ijumaa iliyo pita iliyo tolewa na mwakilishi wake Muheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai- nafasi kubwa na muhimu sana katika vita ya kukomboa ardhi ya Iraq dhidi ya magaidi wa Daesh iliyo ongozwa na jeshi la Iraq kwa kusaidiana na Hashdi Sha’abi (wapiganaji wa kujitolea).

Alionyesha umuhimu wa pekee wa msaada wa raia wa Iraq katika kufanikisha ushindi mkubwa waliopata wanajeshi wetu watukufu na walio pigana nao bega kwa bega miongoni mwa watu walio itikia mwito wa Marjaa dini mkuu wa fatwa ya jihadi ya kujilinda, ambapo alisema kua:

“tunawakumbuka na kuwashukuru sana raia wote wa Iraq walio simama imara na kuwapa misaada mbalimbali wapiganaji watukufu katika uwanja wa vita, hakika walikua ni wasaidizi wema kwa wapiganaji, mlionyesha umoja na mshikamano katika kuwasaidia wapiganaji, pia tunawakumbuka na kumshukuru kila aliye saidia katika sekta ya kutoa elimu, tiba, habari, mashairi, kuandika kitabu, Makala, kipeperushi na vinginevyo. Tunatoa shukrani za dhati kwa kila mtu aliye simama pamoja na wairaq katika kipindi huki kigumu cha mtihani wa magaidi wa Daesh, na kutoa msaada wa aina yeyote, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awaondelee aina zote za shari na awaneemeshe kwa kuwapa amani na usalama”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: