Marjaa dini mkuu: Kuwashinda Daesh hakumaanishi kumalizika kwa vita dhidi ya ugaidi, tunatakiwa kupambana na misingi ya ugaidi kifikra na kidini sambamba na Kuwabana kiuchumi na kihabari…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu katika khutuba ya ushindi ametahadharisha; kuwashinda Daesh isiwe sababu ya kurudi nyuma vita dhidi ya ugaidi, hususan kupambana na njama zao kwani wanatafuta nafasi ya kutekeleza jinai zao, akasisitiza kua ni lazima kupambana na fikra za ubaguzi kutokana na hatari zake kwa wananchi, kwani fikra za ubaguzi haziruhusu watu kuishi kwa amani wala hazikubali mitazamo ya watu wengine na ndio zilizo changia sana kupatikana kwa magaidi wa Daesh.

Hakika Marjaa dini mkuu amechukulia ushindi huu kua ni hatua muhimu ya kihistoria, lakini haimaanishi kumalizika kwa vita dhidi ya ugaidi kwani fikra potofu ni hatari kwa dini na jamii ya kiislamu.

Miongoni mwa usia muhimu alio toa katika khutuba ya ushindi ni umuhimu wa kutengeneza mazingira salama yenye amani, alisema kua: “Hakika kuwashinda magaidi wa Daesh hakumaanshi kuisha kwa vita ya ugaidi, tufahamu wazi vita hii itaendelea madam kuna watu wenye fikra za ubaguzi zisizo kubali kuishi kwa amani na watu wengine wanao tofautiana nao imani na mtazamo, na wala hawaoni vibaya kuua raia wema wasio na hatia au kuteka watoto na wanawake na kuharibu nchi kwa ajili ya kufikia malengo yao mabaya, bali kwa kufanya unyama huo huhisi anajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, tunatakiwa kua na tahadhari sana katika kuamiliana na watu hao hatari wanao endeleza vitendo vya kigaidi, ambao wanaishi nasi wakitafuta nafasi ya kutekeleza ugaidi wao na kuharibu amani na utulivu wa taifa letu.

Hakika tunatakiwa kuendelea kupambana na ugaidi kuanzia katika mizizi yake ya kifikra, kidini na kuhakikisha hawapati wafuasi na kuwabana kiuchumi na kihabari (katika vyombo vya habari), jambo hili linahitaji utafiti wa kina ili kupata mafanikio tarajiwa, kazi ya kulinda usalama na kuimarisha sekta ya upelelezi inahitajika sana, lakini haitoshi lazima iende sambamba na kuonyesha ubaya wa fikra za kigaidi na upotofu wake, na kwamba fikra hizo haziendani kabisa na mafundisho ya dini tukufu ya uislamu, hali kadhalika inatakiwa itolewe mihadhara kwa wingi ya kuhimiza kusameheana na maelewano katika jamii, pamoja na kulipa umuhimu mkubwa swala la kujenga mazingira mazuri ya kuwasaidia wakimbizi kurudi katika miji yao iliyo kombolewa na kuendelea na maisha kwa amani na utulivu na kujenga misingi itakayo saidia kutorejea tena kufanya makossa ya mwanzo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: