Marjaa dini mkuu katika khutuba ya ushindi: Hakika kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kunufaika na wale walio pigana pega kwa bega na wanajeshi wetu watukufu hususan kundi la vijana…

Maoni katika picha
Katika khutuba ya ushindi iliyo tolewa hivi karibuni, Marjaa dini mkuu amewataka wenye mamlaka kutumia nguvu za vijana walio jitolea kulinda taifa lao na maeneo matukufu katika miaka ya hivi karibuni, na wakathibitisha kua wanauwezo wa kutekeleza jukumu hilo, kutokana na ushujaa walio onyesha katika kulinda taifa na imani yao, akiashiria wale walio itikia mwito wa Marjaa wa jihadi ya kujilinda.

Akasema: Hakika jeshi la Iraq bado linahitaji sana vijana mashujaa walio onyesha uwezo wao katika vita, pale walipo ungana na majeshi ya serikali, wakayashinda mazingira magumu ya kivita na kieneo.

Hakika uimara wa mtu, unahitaji uwelewa na ukomavu wa imani, mwenye kuvumilia mazingira magumu katika vita kali lazima awe na moyo imara ulio jengeka kutokana na misingi ya fikra sahihi, haya ndiyo yaliyo sisitizwa na Marjaa dini mkuu siku ya Ijumaa iliyo pita katika khutuba ya ushindi, akasisitiza umuhimu wa kusaidia sekta ya ulinzi na usalama, na akasema jambo hilo ni vizuri likapewa baraka na katika na likawa kisheria, alibainisha kua: “Hakika jeshi la Iraq bado linawahitaji sana watu walio jitolea na kupigana bega kwa bega pamoja nao katika miaka ya hivi karibuni, hakika walikua mstari wa mbele katika kukomboa aridhi ya Iraq na wamethibitisha uwezo wao katika uwanja wa vita, wamepigana vita kali sana katika mazingira magumu, na wamepata ushindi mkubwa ulio shangaza watu wote kitaifa na kimataifa, hususan vijana walio shiriki katika mapambano mbalimbali na katika sekta ya upelelezi na kupata uzowefu mkubwa, walikua mfano mwema katika ushujaa, imani na uzalendo wa taifa lao, hawakurudi nyuma wala hawakuchoka.

Hakika ni muhimu sana kuendekea kunufaika na watu hao chini ya katiba na kanuni ambazo zimeipa mamlaka serikali kuu ya kulinda usalama na kumiliki siraha, watu hawa wasiachwe, tuhakikishe tunawatumia kwa faida ya sasa na ya baadae, na tukae tayali kwa ajili ya kupambana na uvamizi mpya wa magaidi wakati wowote iwapo utatokea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: