Marjaa dini mkuu katika khutuba ya ushindi: Hauwezi kufaulu umma usio lea familia za mashahidi wake walio jitolea uhai wao kwa ajili ya kulinda heshima na utukufu wa watu wao…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa iliyo pita, ameashiria umuhimu wa kuzihudumia familia za mashahidi walio jitolea nafsi zao, na ardhi ya Iraq ikaloa damu zao tukufu kwa ajili ya kuilinda na kulinda maeneo matukufu, akabainisha kua; Mashahidi wana hadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kuhudumia kwetu familia zao ni wajibu wa kizalendo na kimaadili, pia ni jukumu la kidini ambalo tumeachiwa na mashahidi, lazima tuhakikishe familia hizo zinapata maisha mazuri na zinasaidiwa mahitaji muhimu ya maisha yao.

Marjaa akabainisha kua; Serikali na wabunge wana wajibu wa kwanza katika kutekeleza jukumu hili, swala la kutengewa kiwango maalumu cha pesa zitakazo saidia kupunguza ugumu wa maisha lipo ndani ya uwezo wa serikali, hali kadhalika Marjaa dini mkuu katika khutuba yake ya ushindi hakuwasahau walio pata majeraha vitani, miongoni mwa wapiganaji watukufu, kwa hiyo aligusia haki za mashahidi na majeruhi kama ifuatavyo:

“Hakika mashahidi wema walio lowanisha udongo wa Iraq kwa damu zao tukufu, wamekwenda katika maisha ya milele wakiwa wameloa damu, hakika ni utukufu wetu sote, wapo sehemu tukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, jambo dogo sana miongoni mwa wajibu wetu kwao, ni kuzisaidia familia zao, wajane, mayatima na wengineo, hakika kuwatunza watu hao kwa kuwapa mahitaji muhimu katika maisha yao, kama vile; makazi, afya, elimu, na matumizi madogo madogo wanayo hitaji katika maisha ya kila siku ni jukumu wa kiuzalendo na ki-akhlaq, pia ni wajibu wetu sote, hautafanikiwa umma usiojali familia za mashahidi wao walio jitolea maisha kwa ajili yao, jukumu hili kwanza ni la serikali kuu na bunde, wanatakiwa watenge kiasi cha pesa kwa ajili ya kusaidia familia za mashahidi hususan walio pata shahada dhidi ya magaidi wa Daesh, jambo hilo linatakiwa kupewa kipawa mbele zaidi kuliko mambo mengine”.

“Hakika vita dhidi ya magaidi wa Daesh imeacha maelfu ya watu walio pata majeraha vitani miongoni mwa wapiganaji wetu watukufu, wengi wao wanahitaji uangalizi wa kidaktari na wengine wamepata ulemavu wa kudumu, na wengine wamepata ulemavu mbaya mmo, kama vile kupooza mwili mzima, kupoteza macho nk. Watu hawa wanahaki zaidi ya kusaidiwa kuliko mtu mwingine yeyote, hakika utukufu wao ni mkubwa kushinda wairaq wote, kama sio wao Iraq isingekombolewa wala maadui wasinge shindwa, heshima yetu isinge kuwepo wala maeneo matakatifu, hivyo kuwapa mahitaji ya maisha yao na kuhakikisha tunawapunguzia uchungu wao kwa kiasi itakavyo wezekana ni wajibu, inapasa serikali na bunge watenge kiwango cha pesa rasmi kwa ajili hiyo, na swala hili lipewe umuhimu zaidi ya mambo mengine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: