Rais wa miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kua; ujenzi wa kituo cha utamaduni na kusomeshea hatua ya kwanza na ya tatu unaendelea vizuri kwa kiwango kikubwa, pamoja na kuwepo kwa matatizo ya kiuchumi haijawa sababu ya kusimama au kuchelewa kwa ujenzi huo, hii inatokana na juhudi za kampuni inayo tekeleza mradi huu kwa kushirikiana na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wasimamizi wa mradi, kwani wote kwa pamoja wamejitahidi kuondoa vukwazo vyote na kuhakikisha mradi unaenda kama ulivyo pangwa.
Akaongeza kusema kua: “Hakika kampuni inayo tekeleza mradi, ambayo ni kampuni ya Majmu’a Baladawi ya biashara na ujenzi inafanya juhudi kubwa kwa ajili ya kukamilisha mradi, inatumia uwezo wake wote wa rasilimali watu na rasilimali fedha kuhakikisha wanakamilisha mradi huu kama ulivyo pangwa, miongoni mwa mambo yaliyo kamilika ni:
Majengo ya kwanza: Kumaliza ujenzi wa boma la moja ya shule za awali na kuanza kazi ya kukata vyumba kwa kufuata mchoro wa jengo, pamoja na kukamilisha uwekaji wa sistim za (Umeme – vipaza sauti – Ac – Uzimaji wa moto – Tahadhari na zinginezo) pamoja na kukamilisha ujenzi wa vyoo, pia ujenzi wa boma za kumbi mbili za michezo umekamilika bado kujenga paa tu, na ujenzi wa shule nyingine itakayo kua chini ya majengo haya umekamilika katika tabaka la chini bado kuinua tabaka la juu, katika jengo hili kutakua na kituo cha utamaduni, ujenzi wake upo katika ghorofa la kwanza.
Majengo ya tatu: Majengo haya yanahusisha shule tatu, moja katika hizo ujenzi wa boma lake umekamilika na wameanza kazi ya kukata vyumba na kufunga waya za umeme, shule ya pili imekamilika hatua ya msingi na wanaendelea na hatua inayo fuata na shule ya tatu imekamilika kwa asilimia %80, ambambo kuna shule ya awali ambayo imekamilika kwa asilimia %90, kumbi mbili za michezo zilizopo katika majengo haya tayali zimekamilika ujenzi wa boma zake bado paa tu.
Kumbuka kua majengo haya yapo katika barabara ya (Karbala - Hurra) katika eneo lenye ukubwa wa (2m45,000) na yanajumuisha shule tano, kila shule inaeneo lenye ukubwa wa mita za mraba (6000) zenye uwezo wa kubeba wanafunzi wengi sana kwani kila moja ina ghorofa tatu, hali kadhalika kila moja ina shule mbili za awali, zenye ukubwa wa mita za mraba (900) na kumbi mbili za michezo, kila moja ikiwa na ukubwa wa mita (900), zitakazo tumiwa na watumiaji (wanufaika) wa majengo haya, pamoja na majengo hayo ya shule pia kuna jengo maalum la kitengo cha utamaduni ambalo ni alama kubwa ya mradi huu, jengo hilo ni la ghorofa tato na linaukubwa wa mita za mraba elfu (15) ndani ya jengo hilo kuna kumbi za mikutano na ofisi mbalimbali kama zitakavyo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.