Marjaa Sayyid Sistani awaambia wapiganaji wa Hashdi Sha’abi: Kama sio nyie wanawake wangetekwa. Mashahidi wenu wako pamoja na Answari wa Hussein… Wafikishieni mama zenu salam zangu…

Maoni katika picha
(Kama sio nyie wanawake wangetekwa, Hakika mashahidi wenu wako pamoja na Answari wa Hussein (a.s), wafikishieni mama wa mashahidi salam zangu mimi daima nakuombeeni dua kwa Mwenyezi Mungu). Haya yamesemwa na Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani kuwaambia wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) walipo mtembelea wakitanguliwa na kiongozi wao mkuu Shekh Maitham Zaidi na jopo la makamanda wake siku ya Alkhamisi (2 Rabiul-Aakhar 1439h) sawa na (21 Desemba 2017m).

Zoezi hilo liliambatana na kukabidhi bendera ya ushindi kwa Mheshimiwa Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani: Ambayo ni bendera yenye ramani ya Iraq isiyo kua na Daesh, wapiganaji wote waliingia kumsalimia naye alipata furaha kubwa kwa kukutana nao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: