Miongoni mwa harakati zao: Maahadi ya Qur’an tukufu yafanya kisomo cha Qur’an kila wiki katika ukumbi mtukufu wa haram ya Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya imezowea kufanya vikao vya usomaji wa Qur’an, na vinapata mahudhurio makubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara, kutokana na umuhimu wake, hakika Qur’an tukufu hutuliza roho za waumini na huongeza imani pia kutakasa nafsi, Atabatu Abbasiyya tukufu imezowea kufanya vikao vya usomaji wa Qur’an kila wiki katika ukumbi mtukufu wa haram ya Abbasi (a.s).

Vikao vya usomaji wa Qur’an hufanywa kila siku ya Ijumaa kuanzia saa tisa jioni, husimamiwa na idara ya usomaji wa Qur’an ya Maahadi ya Qur’an tukufu, na hushiriki katika vikao hivyo kundi la wanafunzi wa semina za Qur’an zinazo simamiwa na Maahadi ndani na nje ya Karbala, na husoma kwa mahadhi ya kiiraq na kimisri.

Visomo hivyo huhudhuriwa na wanajamii wengi, ambao hutakiwa kikaa kimya kwa unyenyekevu wakati wanapo sikiliza Qur’an tukufu huku wakimfuatisha msomaji kwa sauti za chini.

Tunapenda kufahamisha kua Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya vikao vya usomaji wa Qur’an, semina na mashindano ya Qur’an katika kuadhimisha matukio mbalimbali kwa ajili ya kujenga uwelewa na kusambaza utamaduni wa Qur’an.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: