Kwa kushiriki wanafunzi 160: Atabatu Abbasiyya tukufu yahitimisha hatua ya msingi ya mradi wa kufuta ujinga…

Maoni katika picha
Alasiri ya Juma Mosi (4 Rabiul-Thani 1439h) sawa na (23 Desemba 2017m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ilifanyika hafla ya kuhitimisha hatua ya msingi ya mradi wa kufuta ujinga, unao endeshwa na Atabatu Abbasiyya katika mkoa wa Karbala, kwa kuwasiliana na uongozi wa malezi na kwa kufuata selibasi ya wizara ya malezi ya Iraq.

Hafla ilifunguliwa kwa kuwasikiliza wanafunzi walio faulu katika hatua hii, ambao walisoma Qur’an tukufu kisha ukafuata ujumbe wa msimamizi mkuu wa mradi huu, ulio wasilishwa na Sayyid Muhammad Abduridhwa Mussawiy, akafafanua kua mradi huu ni miongoni mwa miradi ya kitamaduni na kujenga uwezo inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya, unalenga kuwasaidia watu wasio jua kusoma na kuandika, na kuwafanya waweze kusoma na kuandika kwa kiwango cha kuweza kuishi maisha ya kawaida katika ulimwengu huu wa maendeleo na kufuta kabisa tatizo hilo.

Akaongeza kusema kua: “Katika hatua hii walishiriki wanafunzi 160, na wamefaulu wanafunzi 87, wamesomeshwa kwa muda wa miezi sita, katika vituo 11, vituo viwili vilikua chini ya Hashdi Sha’abi na vituo 9 vilifanywa katika Husseiniyya na kumbi ndani na nje ya mkoa wa Karbala, selebasi iliyo fatwa katika ufundishaji ni ileile inayo tumiwa na wizara ya malezi ya Iraq, baada ya kumaliza hatua hii, wataendelea na hatua ya tamhidi, walimu wamefanya juhudi kubwa kuhakikisha hatua hii inaisha kwa mafanikio, tumepata mwitikio mkubwa na ushirikiano mzuri kutoka kwa wanufaika wa mradi jambo ambalo limetushajihisha kuendelea na mradi huu”.

Ustadh Majid Sarhani alitoa shukrani kwa niaba ya kamati ya walimu wa mradi huu, wakiishukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuendesha mradi huu ambao ni msaada mkubwa kwa jamii, unao saidia kuiondoa jamii katika hali fulani na kuipeleka katika hali bora zaidi, pia akawashukuru wanafunzi kutokana na juhudi zao za kujifunza na hamu yao ya kuingia katika hatua ya tamhidi.

Hafla ikahitimishwa kwa kugawa vyeti kwa wanafunzi walio faulu pamoja na walimu wawili wa mradi huu.

Kumbuka kua mradi huu ulianza kutekelezwa baada ya kupata kibali cha wizara ya malezi ya Iraq, na unaendeshwa kwa kushirikiana na ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala chini ya walimu mahiri. Pamoja na kuandaa sehemu maalumu za kusomeshea, ziliandaliwa sehemu za Husseiniyya na kumbi mbalimbali ndani ya mkoa wa Karbala kwa ajili ya kufundishia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: