Kiongozi wa msafara wa Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye ni rais wa kitengo cha dini Shekh Swalahu Karbalai ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Watu wa Sanjaar hususan Aizidiyyin hali yao ni sawa na hali ya miji mingine iliyo kombolewa. Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi na kwa kufuata maelezo ya jaula (misafara) iliyo fanywa hapo awali na kamati ya misaada ya kimkakati ya Ataba tukufu, iliyo leta mapendekezo mfululizo ya umuhimu wa kuja kuwasaidia na kuwaokoa wakazi wa wilaya hii waliopo katika mazingira magumu sana, kutokana na kubomolewa nyumba zao, ugumu wa hali ya hewa na kuwepo wa idadi kubwa ya watoto na wazee waliopo katika mazingira mabaya sana, tuliona umuhimu mkubwa wa kuja kutoa misaada ya kibinadamu katika mji huu, tunatarajia kuwapunguzia japo kidogo matatizo yao kupitia misaada hii”.
Akaongeza kusema kua: “Misaada hii inajumuisha:
- 1- Vikapu vya vyakula mbalimbali, kama vile: Unga, Nyama, Mchele, Sukari, Mayai pamoja na nafaka kavu za aina tofauti.
- 2- Mafuta meupe.
- 3- Vyombo vya kuhifadhia mafuta.
- 4- Nguo za majira ya baridi.
- 5- Kapeti za kutandika chini.
- 6- Magodoro na mashuka.
- 7- Msaada wa pesa.
Karbalai akabainisha kua: “Vilevile muda wote tulipika chakula na kugawa kwa wakazi wa Sanjaar, na tumefunga mtambo wa kutengeneza mikate ambao unatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hali kadhalika tulitembelea maeneo mbalimbali ya mji huo na tumeona uharibifu mkubwa ulio fanywa, pia tulifika hadi katika Maqamu ya bibi Zainabu Sughura (a.s) na malalo ya Ameed Saadah Aarajiin yaliyo bomolewa na Daesh”.
Shekh Karbalai akasisitiza kua: “Hakika sisi tunaendelea kutoa misaada ya kibinadamu lakini sio kwa kiwango kinacho hitajika, hakika mahitaji ni makubwa sana, kuna umuhimu mkubwa wa serikali ifanye haraka kuleta misaada kwa watu hawa sambamba na wale wanao rudi katika miji yao ambayo wanaikuta umebomolewa kabisa”.
Watu wa mji huo wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa misaada hii ya kibinadamu, ambayo waliichukulia kua ni zawadi kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), wakaonyesha kuthamini sana kazi nzuri iliyo fanywa na wahudumu wa msafara huo pamoja na kuvumilia kwao mazingira magumu ya hewa na hali ya kiusalama kwa lengo tu la kuja kuwasaidia.