Kwa namba, hospitali ya rufaa Alkafeel toka kufunguliwa kwake hadi mwezi uliopita imetibu mamia ya watu kwa gharama zake…

Maoni katika picha
Zaidi ya miaka miwili tangu kufunguliwa kwa Hospitali ya rufaa Alkafeel, ndani ya kipindi hicho imepata mafanikio mengi, imepiga hatua kubwa katika utoaji wa matibabu kwa wairaq, kwa namna ambayo imekua ikipigiwa mfano, imetoa huduma kwa watu wa umri tofauti na maradhi mbalimbali, hawakuacha kutoa misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwatibu bure wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi walio jeruhiwa vitani pamoja na familia za mashahidi.

Mkuu wa hospitali hii dokta Haidari Bahadeli amesema kua: “Hakika ndani ya kipindi kilicho pita tumepambana na changamoto kubwa na nyingi katika hospitali yetu, lakini moyo wetu wa kuendelea kutoa huduma sawa na baba kwa wanawe pia kutokana na kujitolea kwa watendaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu tumeweza kushinda changamoto hizo, na tumetoa huduma bora kwa wagonjwa sawa na zile zinazo tolewa na Hospitali za kimataifa katika nchi zingine”.

Akaongeza kusema kua: “Miongoni mwa utaratibu wa utendaji wa idara ya Hospitali, ni kutumia madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka nchi za kiarabu na kiajemi na kuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi, itakayo tufikisha katika lengo kuu ambalo ni kuhakikisha raia wa Iraq hawaendi nje ya nchi kutafuta matibabu, pia tunawapa kipawa mbele zaidi madaktari bingwa wa kiiraq ambao wameonyesha ufanisi mkubwa sana katika utendaji wao”.

Akabainisha kua: “Toka kufunguliwa kwa Hospitali hii hadi mwezi uliopita tumepokea zaidi ya wagonjwa elfu (35), na tumefanya upasuaji zaidi ya (25053) wa magonjwa mbalimbali, madaktari wa kiiraq wamefanya asilimia sabini na tano ya kazi zote zilizo fanyika, huku madaktari wa kigeni wakifanya kazi kwa kiwango kisicho zidi asilimia ishirini na tano, miongoni mwa upasuaji uliofanywa upo ambao sio wa kawaida na nadra sana kufanyika katika Hospitali za Iraq”.

Akaendelea kusema: “Tumefanya upasuaji mkubwa zaidi ya (7750) na upasuaji wa kati (4000) huku upasuaji mdogo ukiwa ni daidi ya (4100), na jumla ya watoto walio zaliwa katika Hospitali yetu ni (3241) huku watoto (367) wakizaliwa kwa njia ya upasuaji”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na Hospitali unaweza kutembelea mtandao wa Hospitali ambao ni: www.kh.iq au piga simu namba: (07602344444) au (07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: