Walio faulu katika shindano la kiongozi wa waumini (a.s): Ndoto yetu ya kutembelea Ataba tukufu za Iraq imefanikiwa…

Maoni katika picha
Baada ya kua, ilikua ndoto kwetu kutembelea malalo matukufu ya Iraq na kuziona kubba takatifu na minara mitukufu, na midomo yetu kubusu madirisha ya makaburi matakatifu, leo kwa utukufu na baraka za mwenye kuhami ardhi ya Iraq na Ataba zake takatifu kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) kupitia kongamano lake tukufu, ndoto hii ambayo ilikua ngumu kwetu hatimae imekamilika.

Haya yamesemwa na mazuwaru walio faulu katika kura iliyo pigwa kwenye shindano lililo fanyika katika kongamano la kiongozi wa waumini (a.s), lililo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Kiongozi wa waumini –a.s- ni hoja kwa waja na muelekezaji katika mema), lililo simamiwa na Ataba za Iraq chini ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa (Kalkata) India, watu 36 walishinda nafasi ya kuja kutembelea Ataba tukufu za Iraq, watu 21 kati yao wamegharamiwa na Atabatu Husseiniyya, watu 5 Atabatu Askariyya na watu 10 wamegharamiwa na Atabatu Abbasiyya.

Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kua ndio wasimamizi wakuu wa kongamano hilo, wamegharamia pia makazi yao katika mji mtukufu wa Karbala na usafiri wa ndani ya mkoa wa Karbala pamoja na usafiri wa kuwapeleka katika Ataba tukufu na maeneo matakatifu yaliyopo Najafu, Bagdadi na Samara kwa kufuata ratiba iliyo andaliwa na kamati ya maandalizi na kusimamiwa na idara ya mahusiano chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuteua watu maalumu walio fuatana na mazuaru hao kuanzia walipo wasili uwanja wa ndege hadi siku watakayo ondoka.

Ratiba yao ilihusisha kutembelea malalo ya kiongozi wa waumini Ali (a.s), Masjid Kufa, malalo ya Kadhimain (a.s), malalo ya Askariyain (a.s) na malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hali kadhalika walitembelea maeneo matukufu mbalimbali yaliyopo ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala pamoja na kuwatembeza katika miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile Hospitali ya rufaa Alkafeel, nyumba za makazi za Abbasi (a.s), vitalu vya Alkafeel pamoja na kuwatembeza katika korido (maeneo) ya Ataba tukufu na vituo vyake vya kutoa huduma.

Mwishoni mwa ratiba hii mazuwaru waliomba dua na kutoa shukrani nyingi wa wasimamizi wa utekelezaji wa ratiba hii kutoka katika kitengo cha mahusiano, wakatoa pia shukrani kwa waandalizi ya kongamano na watumishi wa Ataba tukufu walizo tembelea pamoja na maeneo yote matakatifu waliyo tembelea kutokana na mapokezi mazuri na huduma bora walizo pewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: