Abuu Twalib (r.a) katika macho ya watafiti…

Maoni katika picha
Kwa kusaidiana na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chuo kikuu cha Mustanswiriyya kimefanya nadwa (darasa mjadala) kuhusu (Sayyid Abuu Twalib ni Muumini wa Aali Muhammad -a.s-), washiriki wametoa mada mbalimbali za kitafiti zilizo husu historia ya mtu huyu mtukufu aliye kua na athari kubwa katika uislamu na waislamu, pia walithibitisha upambanaji wake wa pekee, na kua kwake mujahidina (mpambanaji) wa kwanza katika uislamu, muumini wa kikuraishi na msadikishaji wao Abuu Twalib (a.s), Mnusuruji wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mlezi wake, ambaye maadui wa uislamu walijaribu kumchafua kwa njia tofauti, lakini Mwenyezi Mungu mtukufu alikataa na akakamilisha nuru yake hatakama washirikina watachukia, nadwa hii na zingine kama hii ni miongoni mwa juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu zinazo lenga kuonyesha ukweli kuhusu muumini wa kikuraishi na Sayyid Batwihaa Abuu Twalib (r.a).

Sehemu ya nadwa hii ilionyeshwa filamu ya (Mkuu wa maswahaba), iliyo tengenezwa na kituo cha Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nadwa hii imefanyika ndani ya ukumbi wa Farahidi katika chuo tajwa hapo juu, kwa lengo la kuangazia historia ya mpambanaji wa kwanza katika uislamu na kujaribu kuondoa dhulma ya kihistoria aliyo fanyiwa na watu wasio kua na uadilifu katika uhakiki wa kihistoria kwa kujua au kwa chuki tu dhidi ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Dokta Hussein Answari kutoka katika kitivo cha Adabu (Lugha) amebainisha kua: “Hakika picha za video (sinema) zimekua njia muhimu ya mawasiliano na yenye athari kubwa kwa watu, njia hii inatumiwa sana duniani katika makongamano ukizingatia kua tunaishi katika zama za maendeleo na zama za picha, kwa hiyo tunapongeza juhudi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu za kutengeneza filamu zinazo elezea matukio matukufu ya dini ya kiislamu, daima sinema zitaendelea kua njia muhimu ya kufikisha elimu na yenye athari kubwa”.

Ustadh Azhar Khamisi aliye toa maelezo ya filamu hiyo, alisikiliza maoni na maswali ya wahudhuriaji, kisha akatoa ufafanuzi na kujibu maswali.

Watu wote walio hudhuria waliiangalia kwa makini na kuifuatilia kwa karibu filamu hiyo iliyo iliyo chukua muda wa dakika 27, walionyesha kufurahishwa sana na filamu hiyo ambayo ni miongoni mwa matunda ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na wakaomba Ataba iendelee kufanya kazi za aina hii kwa kuibua watu wengine muhimu walio potezwa na historia na kusahalishwa matukufu yao kama mfano wa Abuu Twalib (r.a).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: